Rais William Ruto mchana wa leo anatashuhudia kuapishwa kwa mawaziri waliodhinishwa na bunge siku ya Jumatano.
Hafla hiyo inaandaliwa katika ikulu ya rais mjini Nairobi na kuongozwa na msajili mkuu wa mahakama Anne Amadi.
Viongozi hao walipendekezwa na rais William Ruto kuongoza serikali yake katika baraza la mawaziri na afisi ya rais.
Walipigwa msasa na kamati ya bunge ya uteuzi chini ya Spika Moses Wetangula na kisha kuidhinishwa na bunge la kitaifa.
Mawaziri wanaotarajiwa kuapishwani kama ifuatavyo:
- Mkuu wa Mawaziri Musalia Mudavadi.
- Davis Chirchir (Nishati na Petroli),
- Salim Mvurya (Madini, Uchumi wa majini na Masuala ya Bahari).
- Mercy Wanjau (Katibu wa Baraza la Mawaziri).
- Alfred Mutua (Masuala ya Kigeni).
- Ababu Namwamba (Masuala ya Vijana, Michezo).
- Kipchumba Murkomen (Barabara, Uchukuzi na ujenzi.
- Soipan Tuya (Mazingira na Misitu),
- Njuguna Ndung'u (Hazina ya Kitaifa na Mipango).
- Aliyekuwa Mbunge wa Nyaribari Masaba Ezekiel Machogu (Elimu).
- Eliud Owalo (ICT na Uchumi wa Dijitali)
- Rebecca Miano (Jumuiya ya Afrika Mashariki, Ardhi Kame).
- Florence Bore (Leba na utunzi Jamii).
- Eliud Owalo (ICT na Uchumi wa Dijitali).
- Alice Wahome (Maji).
- Prof Kithure Kindiki (Mambo ya ndani ).
- Moses Kuria (Biashara, Uwekezaji na Viwanda)
- Susan Nakhumicha (Afya. )
- Peninah Malonza (Utalii).
- Justin Muturi (Mwanasheria Mkuu),
- Aden Duale (Ulinzi).
- Simon Chelugui (Ushirika).
Awali kamati ya uteuzi ilikuwa imekataa kuidhinisha jina la Penina Malonza kuwa waziri wa Utalii kwa kile kamati ilitaja kama kutokuwa na ufahamu wa kutosha kuongoza wizra hiyo. Uamuzi wa kamati ya uteuzi hata hivyo ulibatilishwa na bunge la kitaifa.
Upande wa wachache bungeni pia ulikuwa umetaka kuondelawa kwa majina ya Aisha Jumwa na Mithika Linturi baada ya kutilia shaka maadili yao.