logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mwalimu amlipia mwanafunzi safari ya ndege kwa kupata A

Mwalimu aliahidi kuwapandisha ndege wanafunzi ambao wangepata alama ya A

image
na Davis Ojiambo

Habari04 November 2022 - 08:11

Muhtasari


  • • Mwalimu huyo mkuu amekuwa akitumia mbinu mbali mbali kuwapa motisha watahiniwa kabla ya mtihani ya kitaifa kuanza Desemba 2 hadi Desemba 23.
Kijana apata nafasi ya kusafiri kwa ndege baada ya kupata alama ya A

Ni zawadi ipi unaweza kumlipa mwalimu wako wa shule aliyetia bidii usiku kucha ili kukufunza na kukutia maarifa si haba pamoja na kukujengea mustakabali mwema wa maisha?

Katika shule mmoja ya upili huko Kisii, mwalimu mkuu alishabikiwa na watu kutokana na hatua yake kumpeleka mwanafunzi wake kwenye uwanja wa ndege na kumlipia nauli ya ndege.

Inasemekana Mwalimu huyo Fred Magoka alikuwa amewaahidi wanafunzi wake wa kidato cha nne kuwa iwapo wangepata alama alama ya A kwenye mtihani wao wa majaribio basi angewalipia nauli wasafari kwa ndege.

Baada ya mtihani alitimiza ahadi hiyo kwa mwanafunzi huyo ambaye alizoa alama ya A ya alama 81 na kuibuka bora katika shule tano kwenye manispaa ya Kisii.

Mwanafunzi huyo Alex Oyugi na ambaye ni mtahiniwa wa mwaka huu wa kitaifa alipata nafasi ya kusafiri kwa ndege kutoka Kisumu hadi Nairobi na kurudi kabla ya kushiriki kwenye chakula cha mchana jijini.

Mwalimu huyo mkuu amekuwa akitumia mbinu mbali mbali kuwapa motisha watahiniwa kabla ya mtihani ya kitaifa kuanza Desemba 2 hadi Desemba 23.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved