logo

NOW ON AIR

Listen in Live

'Tutapambana na nyinyi,'Mike Sonko awaonya waliomfukuza mjane kutoka kwa nyumba yake ya miaka 46

Kulingana naye, baba mkwe alikufa 2010 na wamekuwa wakiishi katika eneo hilo kwa miaka 46.

image
na Radio Jambo

Habari08 November 2022 - 16:54

Muhtasari


  • Pia aliomba yeyote aliyefahamiana  na familia na mwenye taarifa kuhusu kinachoendelea amtembelee ofisini kwake Upperhill haraka iwezekanavyo
Aliyekuwa gavana wa Nairoi, Mike Sonko

Aliyekuwa Gavana wa Kaunti ya Nairobi, Mike Sonko amegadhabishwa na habari kuhusu kilichompata Mjane Mkenya mwenye asili ya Asia Westlands.

Kulingana na video iliyotangazwa na runinga ya Citizen, mjane huyo alifukuzwa kwa nguvu kutoka kwa nyumba yake ya miaka 46 na mtengenezaji wa kibinafsi aliyedai kumiliki shamba hilo kutoka 2010.

Kulingana naye, baba mkwe alikufa 2010 na wamekuwa wakiishi katika eneo hilo kwa miaka 46.

Runinga ya Citizen ilifichua kuwa kulikuwa na amri ya mahakama iliyomzuia msanidi huyo wa kibinafsi kubomoa nyumba hiyo lakini haikuzingatiwa wakati kitendo hicho cha uhalifu kilipokuwa kikitekelezwa, na hivyo kuacha familia hiyo bila makao.

Ni kutokana na kisa hiki ambapo Mike Sonko alijibu kwa hasira akisema kuwa msanidi  huyo wa kibinafsi atajua kuwa hii si serikali ya Uhuru wakati walikuwa na uhuru wa kufanya lolote.

Pia aliomba yeyote aliyefahamiana  na familia na mwenye taarifa kuhusu kinachoendelea amtembelee ofisini kwake Upperhill haraka iwezekanavyo.

"Naona hii ujinga ya kunyanganya widows properties zao unataka kurudi. Wacha niwaambie nyinyi magrabber mabwenyeye washenzi hii sio serikali ya Uhuru Kenyatta munatumia polisi na magoons kunyanganya wanyonge Mali zao. Tutapambana na nyinyi.Can any one or any close relative of this Asian widow come to my office at upperhill matumbato road opposite pals restaurant with the full details of this sad story we deal with these stupid grabbers ruthlessly,"Sonko Aliandika.

 

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved