logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Winnie Odinga anapaswa kuwa mbunge wa EALA- Robert Alai

Sita hao wanawakilisha kaunti za Mombasa, Wajir, Nairobi, Nyamira, Turkana na Kakamega.

image
na Radio Jambo

Habari11 November 2022 - 12:31

Muhtasari


  • "Familia ya Odinga ni ya kipekee ya kisiasa. Wamefanya mema zaidi kwa Kenya. Mwache Winnie."
  • Wengine walioteuliwa na ODM ni pamoja na mfanyabiashara Suleiman Shahbal, Mohamed Diriye, Timothy Bosire, Beatrice Askul, na Justus Kizito
Mwanablogu na mwanasiasa

Mwakilishi wadi wa Kileleshwa Robert Alai amesema bintiye kiongozi wa Azimio Raila Odinga Winnie Odinga anafaa kuwa na wadhifa wa EALA, si kwa sababu yeye ni bintiye Raila bali kama mtu binafsi.

Winnie ni miongoni mwa wateule sita ambao waliteuliwa na ODM kwa Bunge la Afrika Mashariki.

Katika taarifa yake Ijumaa, Alai alisema Winnie hafai kuadhibiwa kwa sababu anatoka katika ukoo wa Raila.

"Acha Winnie Odinga awe mbunge wa EALA. Alizaliwa mwanasiasa na ni wito wake. EALA ni mwanzo mzuri kwake," alisema.

"Familia ya Odinga ni ya kipekee ya kisiasa. Wamefanya mema zaidi kwa Kenya. Mwache Winnie."

Wengine walioteuliwa na ODM ni pamoja na mfanyabiashara Suleiman Shahbal, Mohamed Diriye, Timothy Bosire, Beatrice Askul, na Justus Kizito.

Sita hao wanawakilisha kaunti za Mombasa, Wajir, Nairobi, Nyamira, Turkana na Kakamega.

 

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved