logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Ugonjwa wa Monkeypox wapewa jina jipya na wataalam wa afya duniani

Jina la zamani litatumika pamoja na hili jipya kwa mwaka mmoja, kabla ya kufutwa.

image
na Radio Jambo

Habari28 November 2022 - 14:44

Muhtasari


  • Mpox iliamuliwa baada ya majadiliano marefu kati ya wataalam, nchi na wananchi kwa ujumla
  • Inaweza kutumika kwa urahisi kwa Kiingereza na lugha zingine, WHO ilisema

Monkeypox sasa imepewa jina la Mpox, Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) limetangaza, baada ya malalamiko juu ya lugha za kibaguzi na unyanyapaa unaohusishwa na jina la virusi hivyo.

Jina la zamani litatumika pamoja na hili jipya kwa mwaka mmoja, kabla ya kufutwa.

Mpox iliamuliwa baada ya majadiliano marefu kati ya wataalam, nchi na wananchi kwa ujumla.

Inaweza kutumika kwa urahisi kwa Kiingereza na lugha zingine, WHO ilisema.

Ugonjwa wa Monkeypox ulitambuliwa kwa mara ya kwanza mnamo 1970 na jina lake kubadilishwa baada ya virusi vyake kugunduliwa miongoni mwa nyani waliozuiliwa kwa zaidi ya miaka kumi klaba ya hapo.

Mwaka huu, umeshuhudia kuenea kusiko kwa kawaida kwa virusi vya mpox - katika nchi nyingi nje ya Afrika ya kati na magharibi, ambapo hupatikana mara nyingi.

Visa vya ugonjwa wa mpox vimeripotiwa katika nchi 29 barani Ulaya, ikiwemo Canada, Australia na Marekani, na kusababisha mahitaji makubwa ya chanjo ya kulinda wale walio katika hatari zaidi.

Mnamo Julai, WHO ilitangaza dharura ya afya ya kimataifa kufuatia ongezeko la watu wanaopata dalili kote duniani, ikiwa ni pamoja na homa kali na vidonda vya ngozi au upele.

 

 

 

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved