logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mwanamke atumia Ksh 280K kwa mwezi kulisha paka 400 chakula mtaani Kayole

Rachael Kibue anaishi na paka hao katika chumba chake cha kulala bila hofu wala wasiwasi.

image
na Davis Ojiambo

Habari13 December 2022 - 13:08

Muhtasari


  • • Kibue amejenga Nairobi Feline Sanctuary ambayo ni makao ya kifahari ya paka.
  • • Alisema paka wake huwa wanamgharimu kati ya ksh 250,000 hadi 280,000 kwa mwezi kwa chakula.
  • • Alisema huwa anaishi na paka hao kwenye chumba chake cha kulala.
Rachael Kibue na paka wake

Wenye midomo husema riziki ya paka imo pipani, lakini kwake Rachael Kibue mwanamke wa kutoka Nairobi, amewapa zaidi ya paka 400 wa kuzurura mitaani makazi na chakula nyumbani kwake Kayole.

Kibue ambaye mapenzi yake kwa paka hayawezi fichika, huwa anawapenda paka sana kiasi cha kuwa amejenga nyumba yenya vyumba vinne ambavyo yeye na paka hao huishi, kula na kulala kwa ustaarabu.

Akizungumza na kituo kimoja cha habari nchini, alisema kuwa huwa anawafuga paka hao ambao anawatoa mitaani na kuwapa makazi mbadala yenye starehe ya chakula na malazi.

"Huwa tunawaokoa watoto wengi wa paka walioachwa kwenye boksi au waliotupwa bila ya mama yao. Huwa wanakosa malezi mema huko nje." alieleza Kibue.

Alisema dhima yake ya kuwa msamaria mwema kwa paka hao, ilimbidi kuanzisha Nairobi Feline Sanctuary - makao spesheli na ya kifahari kwa paka.

Cha kushangaza ni kwamba, Kibue amewapa majina kila mmoja na hawezi kuchanganyikiwa  akiwaita kwa majina.

Licha ya bidii yake ya kuwafuga paka hao, changamoto kuu aliyonayo ni kuwalisha wanyama hao wote kwani gharama ya vyakula huwa ya juu sana.

Alisema huwa anatumia kati ya shilingi 250,00 na 280,000 za Kenya kwa mwezi kuwalisha paka wake. Aliongeza  kuwa anapokea msaada wa chakula kutoka kwa wasamaria wema ila hakitoshi.

"Huwa tunapokea vyakula vya msaada ila havitoshi. Kila wiki paka huwa wanakula kilo 50 ya cabrio na  kilo 70 ya nyama ya kusaga. Kwa mwezi huwa hawakosi kutumia kati ya KSh 250, 000 - KSh 280,000 kwa chakula chao." Kibue alisema kwa mshangao wa wengi.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved