Kilichomuua mwimbaji Ilagosa wa Ilagosa hatimaye chafichuliwa

Mwimbaji wa nyimbo za Injili Ilagosa Wa Ilagosa alifariki dunia kutokana na shinikizo la damu.

Muhtasari

• Ripoti ya daktari ilisema "alifariki kutokana na shinikizo la damu lililosababisha kuongezeka kwa ukubwa wa moyo."

•Atazikwa siku ya Alhamisi.

Ilagosa wa Ilagosa
Image: HISANI

Mwimbaji wa nyimbo za Injili Ilagosa Wa Ilagosa alifariki dunia kutokana na shinikizo la damu.

Familia yake ilifichua kupitia kikundi cha WhatsApp, ambapo marafiki zake wanafanya mchango kwa ajili ya maandalizi ya maziko yake.

Baada ya uchunguzi wa maiti kufanywa siku ya Jumatatu, ripoti ya daktari ilisema "alifariki kutokana na shinikizo la damu lililosababisha kuongezeka kwa ukubwa wa moyo."

Siku ya Jumanne, familia yake na marafiki walikutana katika Hospitali ya St Mary's kwa huduma na kutazama kabla ya mwili wake kuondoka Nairobi kuelekea kaunti ya Vihiga magharibi mwa Kenya.

Atazikwa siku ya Alhamisi.

Bajeti ya mazishi ya Ilagosa ni Sh1.5 milioni. Kufikia sasa, wasanii na marafiki wamechangia zaidi ya Sh500,000 kupitia vikundi vyao viwili vya WhatsApp.

Ilagosa amekuwa akiingia na kutoka hospitalini tangu Desemba 18. Alikuwa amelazwa hospitalini mara mbili kabla ya kulazwa kwa muda mrefu zaidi katika Hospitali ya St Mary's.

Ilagosa ni maarufu kwa wimbo wake wa Sala Zangu, uliotoka miaka mitano iliyopita.

Pia ana collabo zingine na Solomon Mkubwa na Janet Otieno.