Taifa la Misri Kaskazini mwa Afrika linapitia wakati mgumu wa uchumi baada ya kudaiwa kufilisika licha ya kupokea mikopo mingi katika siku za hivi karibuni kutoka IMF.
Kulingana na taarifa za AFP, Misri hivi karibuni walipokea mkopo wa takriban dola bilioni tatu ili kupiga jeki kapu lake la kitaifa lakini bado tatizo la kufilisika linazidi kulitekenya taifa hilo linalotajwa kuwa tajiri Zaidi upande wa Kaskazini mwa Afrika.
Kufuatia kufilisika, Misri wameamua kuuza baadhi ya mali yao ya kitaifa kama mashamba na makampuni kwa mataifa ya Ghuba ili kujikomboa kutoka kwa janga hilo.
Shirika la kimataifa la kutoa mikopo ya hela, IMF lilipotoa mkopo wa dola bilioni 3 kwa Misri, lilionya kwamba taifa hilo huenda litakuwa chini ya msukosuko mkali wa kifedha na katika miaka mine ijayo huenda wakawa na uhaba wa takribani dola bilioni 17.
Mataifa ya Ghuba yakiwemo Kuwait, UAE, Saudi Arabia na mengine yamearifiwa kumezea mate dili hilo la kuuziwa mali za Misri kama njia moja ya kuendeleza ubabe wao katika soko la mafuta ghafi.
“Kwa mataifa ya Ghuba, kushuka kwa kasi kwa thamani ya sarafu ya Misri na vivutio vinavyotolewa na Rais Abdel Fattah al-Sisi vinaifanya kuwa uwekezaji wa kuvutia. Lakini washirika wa Sisi wa Ghuba -- ambao alitegemea msaada wao baada ya kumuondoa madarakani rais wa Kiislamu Mohamed Morsi mwaka 2013 -- wamemaliza kuandika hundi tupu, na sasa wanadai mageuzi ya kiuchumi na uwazi Zaidi,” AFP waliripoti.
Pamoja na hisa katika mikataba 40, kampuni za Imarati na Saudi zilikuwa na shughuli nyingi. Mfuko mkuu wa utajiri wa Abu Dhabi ADQ, na Mfuko wa Uwekezaji wa Umma wa Saudi Arabia "ulitumia dola bilioni 3.1 kupata hisa kubwa za wachache" katika baadhi ya "kampuni zenye nguvu", Enterprise waliandika mnamo Desemba, kulingana na jarida hilo.
Walipata hisa muhimu za wazalishaji wawili wakubwa wa mbolea nchini Misri -- asilimia 41.5 ya Kampuni ya Mbolea ya Abu Qir, na asilimia 45 ya MOPCO.