logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Wabunge wamtembelea mkewe Rigathi Gachagua baada ya kumpoteza dada yake

Mchungaji Dorcas Gachagua alichapisha kwenye ukurasa wake wa Facebook kuhusu habari hiyo

image
na Radio Jambo

Habari22 February 2023 - 11:05

Muhtasari


  • "Mhe. Geoffery Wandeto alinukuu kutoka kitabu cha Ayubu 2:11–13 kuhusu kuwepo kwa wasamaria wema . bu,

Baadhi ya wabunge la kitaifa wamemtembelea mkewe naibu Rais Dorcas Gachagua kumfariji baada ya kumpoteza dada yake Nancy Muthoni Maina.

Kupitia kwenye ukurasa wake rasmi wa Facebook mkewe Naibu Rais alitangaza habari hizo na kuwashukuru viongozi wote waliomtembelea wakati huu wanapitia magumu kama familia.

"Niliguswa na upendo wa wanachama wa Bunge la Kitaifa na Seneti waliokuja kutufariji kufuatia kufiwa na dada yangu, Nancy Muthoni Maina."

Pia alifichua kwamba mbunge wa eneo bunge la Tetu mheshimiwa Geoffrey Wandeto alishiriki kutoka katika kitabu cha Ayubu 2:11-13 kuhusu kuwepo kwa watu wakati wa shida na dhiki, kama marafiki watatu wa Ayubu katika Biblia.

"Mhe. Geoffery Wandeto alishiriki kutoka katika kitabu cha Ayubu 2:11–13 juu ya kuwapo kwa ajili ya watu wakati wa shida na taabu, kama tu marafiki watatu wa Ayubu. Kwa kaka yangu Maina na familia yake, Nakuombea faraja na amani isiyo na mipaka, na mikono yenye huruma ya Mwenyezi Mungu ikushike na kukutia nguvu milele.."

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved