Mahakama ya Juu ya Kenya imeamua kwamba wapenzi wa jinsia moja nchini Kenya ina haki ya kujumuika na kwamba uamuzi wa Bodi ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ya Kenya kuzuia LGBTQ+ kuunda vikundi vinavyotambulika ulikiuka katiba. Hata hivyo, imeonya mahusiano dhidi ya mapenzi ya jinsia moja, ambayo bado ni kinyume cha sheria katika kanuni za adhabu za Kenya.
Mahakama ilisema kuwa licha ya mapenzi ya jinsia moja yameharamishwa nchini Kenya, wanachama wa LGBTQ bado wana haki ya kujumuika.
Kikao cha majaji 5 kilipiga kura 3-2 na kuamua kwamba bodi ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ilikosea kusitisha usajili wa Makundi ya Haki za Kibinadamu ya wapenzi wa jinsia moja mnamo 2013.
Bodi ya Mashirika yasiyo ya Kiserikali iliwasilisha ombi kwa Mahakama ya Juu, baada ya Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufaa kutoa uamuzi dhidi ya uamuzi wao.
Katika rufaa yao ya Mahakama ya Juu, Mkurugenzi Mtendaji wa bodi hiyo alikataa kuidhinisha lolote kati ya majina yaliyopendekezwa kwa misingi kwamba Kifungu cha 162, 163 na 165 cha Kanuni ya Adhabu kinaharamisha uhusiano wa wapenzi wa jinsia moja.
Bodi ya mashirika yasiyo ya kiserikali ilikuwa imekiuka haki ya kundi hilo ya uhuru wa kujumuika chini ya Kifungu cha 36 cha Katiba ya Kenya, ikisema ni ubaguzi na kwamba itakuwa kinyume cha katiba kuweka ukomo wa haki ya kujumuika, kwa kunyimwa usajili. wa chama, kwa misingi ya mwelekeo wa kijinsia wa waombaji.
Uamuzi huo sasa unawapa wapenzi wa jinsia moja uwezo wa kutafuta kutambuliwa rasmi na Bodi ya Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali.
Mnamo Novemba 23, 2021 Mahakama ya Juu ilisikiliza kesi ya kupinga maamuzi ya Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufaa ya kuruhusu Tume ya Kitaifa ya Haki za Kibinadamu za wapenzi wa jinsia mojanchini Kenya (NGLHRC) kusajiliwa rasmi kama shirika lisilo la kiserikali (NGO).