logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Furaha ya Ruto ni kuona Wakikuyu na Wajaluo wakichukiana - Jeremiah Kioni

"Ajenda kuu ya William Ruto ni kuhakikisha kuwa kuna tofauti kati ya Wakikuyu na Wajaluo," Kioni.

image
na Davis Ojiambo

Habari04 March 2023 - 13:40

Muhtasari


  • • Kioni pia alimsifu marehemu Otondi kwa juhudi zake za kuziba pengo la kihistoria lililokuwepo kati ya Wakikuyu na jamii ya Wajaluo.
    • Alidai kuwa Wakenya sasa wanamtazama kiongozi wa upinzani Raila Odinga kuunganisha nchi.

Katibu Mkuu wa Jubilee Jeremiah Kioni amedai kuwa Rais William Ruto ameazimia kueneza uhasama kati ya Wakikuyu na Wajaluo.

Kioni, ambaye alizungumza wakati wa mazishi ya mwenyekiti wa Baraza la Wazee Willis Otondi, alidai kuwa Wakenya sasa wanamtazama kiongozi wa upinzani Raila Odinga kuunganisha nchi.

"Ninataka kusema kwamba ajenda kuu ya William Ruto ni kuhakikisha kuwa kuna tofauti kati ya Wakikuyu na Wajaluo," Kioni alisema.

Mwanachama huyo wa Jubilee aliitaka Jumuiya ya Wajaluo kusimama kidete nyuma ya Raila kwa sababu tayari serikali ya Ruto ya Kenya Kwanza inayumba.

"Wale walio Kenya Kwanza wanakimbia...waliowapigia kura na waliowapinga sasa wanakutazama wewe Baba (Raila)," alisema.

Kioni pia alimsifu marehemu Otondi kwa juhudi zake za kuziba pengo la kihistoria lililokuwepo kati ya Wakikuyu na jamii ya Wajaluo.

"Hata alipokuwa mgonjwa alisafiri mbali na mbali ili kupunguza pengo kati ya Wajaluo na Wakikuyu," alisema.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved