Mahakama ya juu imepeana mwelekeo wa kusikizwa kwa kesi ya naibu rais Rigathi Gachagua tarehe 16 machi mwaka huu.Naibu rais anapigania kurejesha mali yenye thamani ya shilingi bilioni 1.5 iliyoko karibu na uwanja wa ndege wa JKIA.
Kesi hiyo ilikuwa isikilizwe tarehe 9 Machi lakini mahakama iliarifiwa kuwa wakili wake Gachagua alikuwa anajihisi vibaya kiasi.Kutokana na hili hakimu Justice Ogutu Mboya alimpa Gachagua faini ya shilingi elfu tano.
"Mlalamikaji atalipa ada ya kuahirisha mahakama ya 5000 inayolipwa kwa Hazina ya Kitaifa ndani ya siku saba bila kushindwa hatakuwa na haki ya kusikizwa," aliamuru Jaji.
Katika kesi hiyo DP kupitia kampuni yake ya Wamunyoro Investments inamshtumu Ohas kwa kupata hati miliki ya ardhi hiyo kinyume cha sheria mnamo Desemba 2019 na kuisajili kwa jina la kampuni yake.
Mahakama ilisikia kwamba kampuni ya Ohas ya Columbus Two Thousand Limited inanuia kumbadilisha kama shahidi mkuu kwa vile alikuwa mgonjwa.
"Tunaweza kufikiria kuchukua nafasi ya Michael John Ohas ambaye ni shahidi mkuu, kwa kuwa amekuwa mgonjwa kwa muda na amelazwa hospitali hivi majuzi," wakili anayewakilisha kampuni hiyo aliambia mahakama.
Jaji Mboya aliagiza ombi hilo lifanywe kwa wakati ufaao na kuahirisha kesi hiyo hadi Machi 16.