logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Waziri wa Utalii,Peninah Malonza abatilisha uteuzi wa Pauline Njoroge kama mwanachama wa bodi ya utalii

Waziri wa Utalii, alibatilisha uteuzi wa Pauline Njoroge kutoka bodi ya Utalii.

image
na Davis Ojiambo

Habari10 March 2023 - 12:37

Muhtasari


  • • Ni mara ya pili uteuzi wa Pauline  umebatilishwa katika bodi ya utalii.

 Waziri wa Utalii,Peninah Malonza amebatilisha uteuzi wa Pauline Njoroge kama mjumbe wa bodi.

Njoroge aliteuliwa mwaka  2020 kuhudumu katika bodi ya utalii na aliyekuwa waziri wa Utalii Najib Balala. Hata hivyo siku ya Alhamisi Njoroge alikuwa miongoni mwa wanachama watano wa bodi hiyo waliopigwa kalamu na Malonza. 

Wengine ambao uteuzi wao ulibatilishwa ni Kevin Muasya, Najma Ismail, Alais Lenana Momoi na Isaac Muchiri Njangu.

Pauline Njoroge amekuwa kwenye mstari wa mbele kuishutumu serikali ya Kenya Kwanza.

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved