logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Raila atishia kumshtaki Rais Ruto,atoa sababu

Waziri Mkuu huyo wa zamani mnamo Alhamisi alipeleka kampeni zake za kupinga serikali hadi Nakuru.

image
na Radio Jambo

Habari16 March 2023 - 13:01

Muhtasari


  • Akizungumza mjini Nakuru siku ya Alhamisi, Raila alisema aliondolewa mashtaka ya uhaini, lakini Ruto ameendelea kuharibu jina lake

Kiongozi wa Azimio Raila Odinga sasa anasema kwamba atamshtaki Rais William Ruto kwa kumharibia jina.

Akizungumza mjini Nakuru siku ya Alhamisi, Raila alisema aliondolewa mashtaka ya uhaini, lakini Ruto ameendelea kuharibu jina lake.

Alisema mahakama haikupata ushahidi wowote kwamba alishiriki katika jaribio la 1982 la kupindua serikali ya Rais wa zamani Daniel Moi.

“Niliondolewa mashtaka ya uhaini baada ya mahakama kugundua kuwa hakuna ushahidi ulionihusisha na jaribio la mapinduzi ya 1982. Ruto ameharibu jina langu na nitaenda kumshtaki kwa kunichafuliwa jina,” alisema.

Alisema kuwa serikali ya wakati huo ilimzuilia katika Gereza la Kamiti Maximum kwa miezi sita alipokuwa akikabiliwa na mashtaka mahakamani, lakini akashinda kesi hiyo mwaka wa 1983.

Waziri Mkuu huyo wa zamani mnamo Alhamisi alipeleka kampeni zake za kupinga serikali hadi Nakuru.

Aliandamana na kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka na kiongozi wa DAPK Eugene Wamalwa miongoni mwa wengine.

 

 

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved