Muuaji aliyevamia shule la chekechea na kuwaua wanafunzi kadhaa na wafanyikazi wa shule nchini Marekani hatimaye ametambulika pamoja na mazungumzo yake ya mwisho na rafiki yake.
Vyobo vya habari mapema Jumanne viliripoti nchini humo kuhusu tukio hilo la uvamizi shuleni na mtu huyo mwenye jinsia ya kiume ambaye alikuwa anajitambua kama shoga wa jinsia mbili alivamia shule ya watoto wa chekechea akiwa na bunduki.
Rafiki yake wa karibu ambaye walifanya mazungumzo ya mwisho naye ambapo jamaa muuaji huyo kwa jina Audrey Hale mwenye umri wa miaka 28 alimhakikishia rafiki yake kuwa angemsikia katika vyombo vya habari baada ya kufa akitekeleza kitendo hicho cha uchungu kwa watoto.
“Kwa hivyo kimsingi chapisho hilo nililoandika hapa kuhusu wewe, kimsingi lilikuwa barua ya kujiua. Ninapanga kufa leo,” Hale aliandika, akitumia jina la Aiden, kulingana na ujumbe ambao rafiki yake Patton alitoa kwa vyombo vya dola.
“HUU SI UTANI!!!” aliandika Hale, ambaye alijitambulisha kama mtu aliyebadili jinsia. "Labda utasikia juu yangu kwenye habari baada ya kufa."
Hale aliongeza: “Hii ni kwaheri yangu ya mwisho. Nakupenda… Tuonane tena katika maisha mengine.”
Hata hivyo, rafiki yake huyo alijaribu kumbembeleza alifanye uamuzi huo lakini Audrey alikuwa mtu aliyekuwa na akili yake imefanya uamuzi usiobadilika.
Alisisitiza kwamba hataki kuishi kwa vile familia yake imemtelekeza.
“Najua lakini sitaki kuishi. Samahani. Sijaribu kukukasirisha au kupata umakini. Nahitaji kufa tu. Nilitaka kukuambia kwanza kwa sababu wewe ndiye mrembo zaidi ambaye nimewahi kuona na kumjua maisha yangu yote.”
Dakika chache baadae, video ya CCTV ilimuonesha muuaji huyo akiendesha gari dogo kuelekea shule hiyo kabla ya kukimbia akiwa amenyoosha mtutu wa bunduki tayari kufanya maangamizi.
Alivunja vioo vya madirisha ya milango huku akilazimisha kuingia ndani.
Aliwapiga risasi watoto watatu wa miaka 9 na wafanyakazi watatu kabla ya kuuawa kwa kupigwa risasi na polisi saa mwendo was aa nne na nusu asubuhi - dakika 14 baada ya polisi kupokea simu kuhusu tukio hilo.