Inspekta Jenerali Japhet Koome amesema kuwa afisa mmoja wa polisi aliuawa wakati wa maandamano ya kupinga serikali yaliyoongozwa na Raila Odinga siku ya Alhamisi.
Katika taarifa yake, Koome alilaani vitendo hivyo vya kinyama, akisisitiza kuwa uchunguzi kuhusu matukio hayo umeanzishwa.
“Kutokana na maandamano ya jana, afisa mmoja wa polisi mjini Kisumu alifariki kutokana na majeraha aliyoyapata akiwa kazini, maafisa 20 walijeruhiwa vibaya walipokabiliana na waandamanaji...Mali ambayo thamani yake bado haijabainishwa iliharibiwa baada ya waandamanaji kuvamia mali ya kibinafsi," alisema.
Koome alihakikishia umma usalama wao akisema kuwa polisi watafanya kila wawezalo kuwalinda.