logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Aliyekuwa kiongozi wa Mungiki, Maina Njenga anasakwa - DCI

Amin alisema vitu hivyo vilipatikana kufuatia msako mkali wa wapelelezi katika kijiji cha Ngomongo, eneo la Dundori.

image
na Samuel Maina

Habari23 May 2023 - 04:07

Muhtasari


  • •Njenga anasakwa kuhusiana na bunduki mbili na zaidi ya misokoto 90 ya bangi iliyopatikana kwa nyumba inayohusishwa naye.
  • •Mnamo Mei 12, Njenga alidai kuwa nyumba zake tatu huko Nairobi, Nakuru na Laikipia zilivamiwa na polisi.
Maina Njenga

Maafisa wa upelelezi kaunti ya Nakuru wanamsaka aliyekuwa kiongozi wa Mungiki Maina Njenga kuhusiana na kupatikana kwa bunduki mbili na zaidi ya misokoto 90 ya bangi katika nyumba inayohusishwa naye.

"Moja ya bunduki zilizopatikana ni bastola ya kujitengenezea nyumbani iliyokuwa na uwezo wa kufyatua huku nyingine ikiwa ni Tokarev ambayo nambari yake ya usajili ilikuwa imeharibiwa."

Mkuu wa DCI Mohamed Amin alisema katika taarifa yake Jumatatu jioni kwamba vitu hivyo vilipatikana kufuatia msako mkali wa wapelelezi katika kijiji cha Ngomongo, eneo la Dundori.

Alisema risasi tatu za 9mm tupu pia zilikutwa zikiwa zimefichwa kwenye moja ya vyumba ndani ya nyumba hiyo.

Amin alisema maafisa hao waliwakamata washukiwa wanane wenye umri wa kati ya miaka 37 na 54 wakati wa msako huo.

"Taarifa yoyote kuhusu aliko kiongozi huyo wa zamani wa Mungiki ambaye huenda amejificha inaweza kutolewa kupitia nambari ya simu ya #FichuakwaDCI 0800 722 203," Amin alisema.

Mnamo Mei 12, Njenga alidai kuwa nyumba zake tatu huko Nairobi, Nakuru na Laikipia zilivamiwa na polisi.

Alisema timu hizo, ambazo zilifika kwa wakati mmoja saa kumi asubuhi nyumbani kwake Lavington, Karen na Nyandarua, ziliwaambia wafanyakazi kuwa walikuwa wakimtafuta.

Baadhi ya wafanyikazi katika makazi yake ya Nyahururu waliambia vyombo vya habari kuwa takriban maafisa 20 walivamia nyumba hiyo na kutaka kupekua nyumba hiyo.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved