Kiongozi wa chama cha Orange democratic movement (ODM) Mhe Raila Odinga amesema kuwa hatua yoyote ya washirika wa rais William Ruto kumtimua rais wa zamani Uhuru Kenyatta kutoka chama cha Jubilee haitafaulu.
Kulingana naye chama cha Jubilee ni cha Azimio La Umoja chama kimoja cha muungano huo baada ya kutia saini makubaliano kabla ya uchaguzi mkuu wa 2022.
Raila aliweka wazi Kwamba wako tayari kutetea chama cha Jubilee kwa sababu ni chao.
"UDA ilikuwa na vyama vyao ambavyo vilijiunga nao kwa ihari,Azimio pia ilikuwa na vyama ambavyo walijiunga nasi kwa ihari,Tulilipa mahari ya chama cha Jubilee, ni yetu wanataka kununua wabunge wa Jbileelakini hawatafauli" Alisema Raila Odinga kiongozi wa chama cha Azimio.
Akizungumza wakati wa ibada ya shukrani na maombi ya Kalonzo Musyoka katika shamba lake la Yatta kaunti ya Kitui kiongozi wa upinzani Raila Odinga alisema kuwa Mswada wa Fedha ni dharau kwa Wakenya.
"Mswada wa Sheria ya Fedha wa 2023 ni dharau kwa Wakenya. Tayari watu wanatatizika kupata riziki, na sasa wao (gov’t) wanaongeza ushuru bila ya kuadhibiwa. Hakutakuwa na ushuru bila uwakilishi". Alisema Raila Odinga
Kiongozi wa Azimio Raila Odinga pia ametoa changamoto kwa Rais William Ruto kutafuta mafunzo kutoka kwake kuhusu ushuru wa Hazina ya Nyumba.
Raila alishutumu serikali kwa kuwaelemea Wakenya wakati ambapo nchi inatatizika kiuchumi.
Bosi huyo wa Upinzani alisema kwamba Ushuru wa Nyumba ni dharau kwa Wakenya na akasema alipaswa kushauriwa kwa vile anajua zaidi kuhusu Ushuru wa Nyumba.
"Nina ujuzi wa Housing Levy, walipaswa kuja kwangu kwa masomo. Ningewafundisha kwa sababu hawajui," Raila alisema.
"Huwezi kuanzisha ushuru wa ziada wakati uchumi umeshuka, huwezi kufanya hivyo. Ulipata wapi asilimia tatu? Ikiwa unasema ni uwekezaji, vipi kuhusu mwajiri? Mwajiri anawekeza nini? ndani?"
Kiongozi huyo wa ODM alisema ushuru wa ziada wa asilimia tatu kwa mwajiri hauwezi kudumu.
Raila alishikilia kuwa hakutakuwa na ushuru kwa Wakenya bila uwakilishi.