logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mackenzie na wenzake wasusia mlo kufuatia matamshi ya Kindiki

Washukiwa hao walidai kuwa mashtaka yameamua hatima yao, na hawatapata haki katika kesi inayoendelea.

image
na Radio Jambo

Habari07 June 2023 - 15:15

Muhtasari


  • Mhubiri huyo wa Kanisa la Good New International Church alishangaa kwa nini Kindiki aliharakisha kumhukumu kifungo cha maisha, lakini Serikali haikuwa imemfungulia mashtaka.
katika mahakama ya Shanzu mnamo Juni 2, 2023

Paul Mackenzie wa Kanisa la Good News International Church na washtakiwa wenzake, akiwemo mkewe, Rhodah Mumbua, Jumatano, Juni 7, walianza mgomo wa kula gerezani.

Kulingana na wakili wao, Mackenzie, mkewe na washukiwa wengine walikasirishwa na tishio la Waziri wa Usalama wa Ndani Kithure Kindiki kwamba atahakikisha pasta huyo anasalia gerezani maisha yote.

Washukiwa hao walidai kuwa mashtaka yameamua hatima yao, na hawatapata haki katika kesi inayoendelea.

"Tunahitaji uhakikisho fulani kutoka kwa Jaji Mkuu Mheshimiwa Martha Koome kwamba mteja wetu atapata haki wakati wa kesi hii," wakili wa Mackenzie aliomba.

Wakili huyo alidai kuwa wateja wake wangesali na kufunga hadi wakati ambapo Kindiki anatengua kauli yake.

Mhubiri huyo wa Kanisa la Good New International Church alishangaa kwa nini Kindiki aliharakisha kumhukumu kifungo cha maisha, lakini Serikali haikuwa imemfungulia mashtaka.

"Tunaona uwezekano wa kuharibika kwa haki kwa vile mtu aliyezungumza ni mtu aliyewekwa nafasi ya juu na mwenye uwezo mkubwa," wakili wa Mackenzie alisema.

Akihutubia Ibada ya Kanisa katika Kanisa la Kenya Assemblies of God huko Sagana, Kirinyaga, Jumapili, Juni 5, Kindiki alisema kwamba mhubiri mwenye utata Paul Mackenzie angefungwa maisha kwa kuwa uhalifu wake ulifikia kifungo cha maisha.

"Mackenzie hatatoka jela, atazeeka ndani yake. Tunaomba Mungu ampe miaka mingi zaidi ili kuona usalama wa Kenya ukiimarika.

Hatatoka jela... Mackenzie atakutana na ghadhabu ya Mungu baada ya jela," Kindiki alisema.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved