Mtu mmoja anayedhaniwa kuwa mfuasi wa mhubiri tata Paul Mackenzie ameripotiwa kufariki akiwa katka kizuizi cha polisi baada ya kile kilitajwa kuwa ni njaa ya siku kumi.
Jarida la Nation liliripoti kwamba wengine wawili walikimbizwa hospitali wakiwa katika hali mbaya ya afya.
“Tunashuku marehemu alifariki kutokana na njaa ya chakula. Kwa sasa tusubiri tu uchunguzi wa maiti ili kubaini chanzo cha kifo,” mwendesha mashtaka aliiambia mahakama kama alivyonukuliwa na jarida la Nation.
Mtu huyo aliyefariki alitajwa kwa jina Juma Joseph Buyuka na alikuwa miongoni mwa watu 30 ambao walikuwa wamehamishwa kwenda gerezani baada ya kuanzisha mgomo wa kutokula wakiwa kwenye seli.
Mahakama iliambiwa kwamba marehemu alipelekwa katika hospitali ya Malindi baada ya afya yake kudhoofika akiwa gerezani.
Wiki jana watu hao walifikishwa mahakamani wakiwa katika hali ya kutia huruma ambapo mahakama ilisema wahamishiwe magereza na kuwekwa chini ya mpango wa kulazimishiwa chakula ili kuimarisha hali yao kabla ya kushtakiwa.
Kudikia sasa, shughuli ya ufukuaji maiti ambayo imesitishwa wiki jana imeona maiti Zaidi ya 300 ikifukuliwa katika shamba la Shakahola.
Mchungaji Paul Mackenzi anazuiliwa na atafunguliwa mashtaka ya mauaji y halaiki.
Waumini hao wengi ambao walifariki na miili yao kufanyiwa uchunguzi baada ya kufukuliwa ilionyesha dalili za kufa kutokana na kukosa chakula na maji.
Mackenzie anaarifiwa kuwataka waumini wake kujitesa hadi kufa kama njia moja ya kuwapa uhakikisho wa kukutana na Yesu.