Aliyekuwa gavana wa kaunti ya Nairobi Mike Sonko amezungumza kuhusu video inayosambaa katika mtandao wa TikTok, kuhusu mtoto aliyeokolewa na wanaume wenye huruma, aliyekuwa ametupwa katika shimo la choo.
Kulingana na Sonko, mtoto aliyeokolewa alikuwa ametupwa ndani ya shimo hilo na mamake mapema asubuhi ya Juni 23.
Katika mtandao wake wa Twitter, aliposti kuwa iwapo mabinti wameshindwa kuwaelea watoto wao badala ya kuwadhulumu wampeleke kwake na kuwa yupo tayari kuwatunza.
“Huyu mtoto alipatikana asubuhi kama ametupwa kwa choo na mamake. I've said it before na nitasema tena, madem mkifeel hamuezi kulea watoi msiwadhulumu kivyovote, waleteni kwangu nitawalea vizuri.”
Huyu mtoto alipatikana asubui kama ametupwa kwa choo na mamake. I've said it before na nitasema tena, madem mkifeel hamuezi kulea watoi msiwadhulumu kivyovote, waleteni kwangu nitawalea vizuri. pic.twitter.com/kwmZbTIUvp
— Mike Sonko (@MikeSonko) June 23, 2023
Aliposti haya ambayo katika tafsiri ni kuwa; Nimesema hili awali, na nitasema tena, wasichana mkijihisi hamuwezi kulea watoto msiwadhulumu kivyovyote, waleteni kwangu na nitawalea vizuri.
Kulingana na kauli ya Sonko, mtoto huyo kwa bahati nzuri yupo hai, ambapo alikashifu vikali tendo la wasichana kutowajibikia watoto wao.
Haya yanajiri wakati ambapo mwanasiasa huyo ameonekana kuwasaidia watu wengi, hasa alipoahidi kumtunza mtoto mmoja katika shule ya msingi katika kaunti ya Narok, aliyenaswa akishonewa sare yake ya shule iliyochanika na mwalimu wake darasani, pamoja na kumpa kazi aliyekuwa mchezaji wa mashindano ya dondi Conjestina.