Mmiliki wa Facebook, Meta imeeleza mpango wake wa kuzindua programu mpya siku ya Alhamisi ili kuweza kuleta upinzani kwa mtandao wa Twitter.
Programu hiyo, inayoitwa Threads na inapatikana kwa kuagiza mapema kwenye Apple App Store, itaunganishwa na programu nyingine inayomilikiwa n kampuni hiyo hiyo, Instagram.
Meta inafafanua Threads kama "programu ya mazungumzo ya maandishi".
Hatua hiyo ni ya hivi punde ya ushindani kati ya bosi wa Meta Mark Zuckerberg na mmiliki wa Twitter Elon Musk.
Jumamosi, Twitter iliweka kikomo cha muda kwa idadi ya tweets watumiaji wanaweza kusoma kwa siku, mmiliki Elon Musk alisema.
Katika tweet yake mwenyewe, Bw Musk alisema akaunti ambazo hazijathibitishwa sasa ni za kusoma machapisho 1,000 kwa siku.
Kwa akaunti mpya ambazo hazijathibitishwa, nambari ni 500. Wakati huo huo, akaunti zilizo na hali "zilizothibitishwa" kwa sasa zimezuiwa kwa machapisho 10,000 kwa siku.