logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Watu 5 wauawa kwa kupigwa risasi wakati wa maandamano Mlolongo, Kitengela

Polisi wanasema kuwa waandamanaji hao ambao wanadaiwa pia kurusha mawe kwenye Duka Kuu la Quick Mart

image
na Radio Jambo

Michezo12 July 2023 - 14:13

Muhtasari


  • Watu watatu kati ya waliofariki waliuawa kwa kupigwa risasi karibu na Kituo express way cha Mlolongo baada ya kuziba na kuharibu barabara

Watu watano waliuawa Jumatano katika makabiliano tofauti kati ya polisi na waandamanaji wanaoipinga serikali katika Kaunti za Machakos na Kajiado.

Watu watatu kati ya waliofariki waliuawa kwa kupigwa risasi karibu na Kituo express way cha Mlolongo baada ya kuziba na kuharibu barabara jambo ambalo lilisababisha msongamano wa magari katika njia hiyo.

Polisi wanasema kuwa waandamanaji hao ambao wanadaiwa pia kurusha mawe kwenye Duka Kuu la Quick Mart lililo karibu na kituo cha ushuru, walitaka kupora duka hilo baada ya kuharibu ukuta wa Barabara ya Mlolongo.

Polisi hata hivyo wamekilinda kitengo cha miundombinu muhimu na kufunga barabara ya mwendokasi, na hivyo kusababisha msongamano wa magari katika njia inayounganisha Mlolongo hadi Nairobi.

Majeruhi wawili waliosalia vile vile walipoteza maisha yao katika maandamano sawa huko Kitengela.

Kwenye video zilizoonekana na Radiojambo waandamanji wanaonekana wakiwa na ghadhabu huku wakibomoa sehemu ya barabara ya Express Way Mlolongo kaunti ya Machakos.

Hata hivyo IG Koome alisema kuwa maandamano ambayo yaliitishwa na muungano wa Azimio sio halali.

 

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved