Gavana wa Nairobi, Johnson Sakaja amefanyia mabadiliko baraza lake la mawaziri katika kaunti la Nairobi miezi saba tu baada ya kuapishwa.
Katika taarifa kwenye vyombo vya habari, Sakaja alisema hatua hiyo ilifanyika kwa mujibu wa sheria ya usimamizi wa kaunti.
Mawaziri nane kati ya kumi walibadilishwa kutoka wizara walizokuwa wakiongoza na kupewa wizara mpya.
Baadhi ya mabadiliko hayo ni waziri wa maswala ya mazingira, Suzanne Njeri amehamishwa kulekea wizara ya Biashara na fursa za Mahustler wa kaunti ya Nairobi. Naye Ibrahim Auma akichukua pahali pake katika wizara ya mazingira kutoka kwa wizara ya utawala na wafanyakazi.
Waziri wa ushiriki wa umma na huduma kwa wateja, Suzanne Silantoi akichukua hatamu katika wizara ya Afya na lishe. Nafasi iliyoongozwa na waziri Anastasia Nyalita huku nyalita akihamia wizara hiyo iliyoongozwa na Silantoi.
Bw. Patrick Mbogo sasa atachukua ofisi ya wizara ya utawala na wafanyakazi wa kaunti kutoka kwa wizara ya barabara.
Waziri wa maswala ya biashara, Rosemary Kariuki sasa ndiye waziri wa talanta na ujuzi, huku akiachiwa ofisi hiyo na Brian Mulama ambaye ameelekea katika wizara ya barabara.
Waziri Charles Kerich na Bw. Michael Gumo ndio mawaziri pekee ambao hawakuhamishwa wakisalia katika wizara ya fedha na wizara ya ubunifu na uchumi wa kidijitali mtawalia.
Aidha, Sakaja aliwajumuisha Daktari Stephen Gchie na Bernard Kioko kama washauri wake.
Stephen anajuinga na jumba la City Hall kama mshauri wa maswala ya uchumi naye Bernard kuwa msauri wake wa kibinafsi kuhusiana na uchumi wa ubunifu.