logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Genge lashambulia treni ya Nairobi iliyokuwa na wanafunzi 520

"Tungependa kuwafahamisha wateja wetu na umma kwa ujumla kwamba tumesitisha huduma za treni

image
na Radio Jambo

Habari13 July 2023 - 13:38

Muhtasari


  • Genge hilo liliirushia treni mawe na kuziba njia, na hivyo kuweka maisha ya watu waliokuwemo hatarini.
  • Tukio jingine lilitokea Jumatano, Julai 12, saa 12:00 usiku ambapo washambuliaji walilenga treni iliyokuwa ikielekea Lukenya.

Shirika la Reli la Kenya mnamo Alhamisi, Julai 13, lilisitisha huduma za treni  Syokimau na Lukenya kufuatia visa viwili ambapo magaidi wasiojulikana walishambulia treni, na kuhatarisha maisha ya abiria.

Shirika hilo lilifichua mnamo Alhamisi kwamba mwendo wa saa 11:00 asubuhi, kundi la vijana waliokuwa na ghasia walivamia treni iliyokuwa na wanafunzi 520 kwenye njia ya Mukuru kwa Njenga.

Genge hilo liliirushia treni mawe na kuziba njia, na hivyo kuweka maisha ya watu waliokuwemo hatarini.

Tukio jingine lilitokea Jumatano, Julai 12, saa 12:00 usiku ambapo washambuliaji walilenga treni iliyokuwa ikielekea Lukenya.

Shirika la Reli la Kenya halikufichua ikiwa wanafunzi waliokuwemo walijeruhiwa wakati wa kisa hicho cha asubuhi.

"Tungependa kuwafahamisha wateja wetu na umma kwa ujumla kwamba tumesitisha huduma za treni kwenye njia ya Syokimau na Lukenya.

"Hii ni kutokana na hali tete ya usalama inayotokana na mashambulizi ya mara kwa mara kwenye treni zetu zinazopitia Mukuru kwa Njenga, na watu wenye ghasia ambao wanazuia njia za reli na kuipiga kwa mawe treni," taarifa hiyo ilisoma kwa sehemu.

"Tunaangazia matukio mawili ambapo, jana jioni, treni ya Lukenya ilivamiwa saa 6:00 usiku, na asubuhi ya leo, treni iliyokuwa na wanafunzi 520 ilishambuliwa saa 11:00. Tunataka kusisitiza kwamba usalama wa abiria wetu bado. muhimu kwetu."

Shirika la Reli la Kenya lilithibitisha kuwa taarifa rasmi itatolewa mara huduma za kawaida zitakaporejea.

 

 

 

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved