logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Watu 2 wamefariki na 52 kujeruhiwa katika ajali iliyotokea Barabara kuu ya Nairobi - Nakuru

Polisi walisema wanafunzi hao walikimbizwa na kulazwa katika Hospitali ya PCEA Kikuyu.

image
na Davis Ojiambo

Habari15 July 2023 - 13:30

Muhtasari


  • • Miongoni mwa waliojeruhiwa ni wanafunzi wawili wa Shule ya Sekondari ya Twilight iliyoko Kayole, Kaunti ya Nairobi.
  • •  Polisi walisema wanafunzi hao walikimbizwa na kulazwa katika Hospitali ya PCEA Kikuyu.
  •  

Takriban watu wawili walifariki huku makumi ya wengine wakijeruhiwa kufuatia ajali ya barabarani eneo la Muguga kwenye barabara kuu ya Nairobi-Nakuru Ijumaa usiku.

Polisi walisema kasisi mmoja na mkewe walifariki papo hapo baada ya trela lililokuwa na hitilafu ya breki kugonga gari lao katika ajali hiyo ambapo magari 20 yalihusika, likiwemo basi la shule lililokuwa na wanafunzi 44.

Miongoni mwa waliojeruhiwa ni wanafunzi wawili wa Shule ya Sekondari ya Twilight iliyoko Kayole, Kaunti ya Nairobi.

Polisi walisema wanafunzi hao walikimbizwa na kulazwa katika Hospitali ya PCEA Kikuyu.

Kamanda wa Polisi wa kaunti ndogo ya Kikuyu Ronald Kirui alisema wengine wengi waliojeruhiwa walipelekwa hospitalini.

Alisema uchunguzi wa tukio hilo unaendelea.

Aliwaambia madereva kudumisha nidhamu ya udereva na kuhudumia magari yao ikiwa ni sehemu ya juhudi za kukabiliana na ajali hizo.

Wenyeji walizitaka mamlaka husika zinazoongozwa na KeNHA kukamilisha sehemu ya barabara ambapo njia za kutoa huduma zitajengwa ili kuepusha hasara zaidi ya maisha.

Visa vya ajali mbaya vimeongezeka licha ya kampeni za kukabiliana na tishio hilo.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved