Klabu ya Saudi Arabia, Al Hilal imewasilisha dau la pauni milioni 259 (Ksh 47.2B) kwa PSG ili kumnunua mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe.
Miamba hao wa Ufaransa ambao hawajakuwa katika uhusiano mzuri na mshambuliaji huyo wameripotiwa kukubali ombi hilo la kuvutia na kukubali kumuuza.
Hata hivyo, Al Hilal bado haijaanza mazungumzo na Mbappe mwenyewe kama ripoti kutoka Ulaya zinavyoonyesha. Iwapo nahodha huyo wa timu ya taifa ya Ufaransa atakubali uhamisho huo, basi atakuwa mchezaji ghali zaidi wa soka wa wakati wote.
Al Hilal imeripotiwa kuandaa ofa nzuri ya mshahara kwa mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 24 huku wakisemekana kuwa tayari kumlipa bilioni 9.2 kwa mwezi. Hii ni kumaanisha mchezaji huyo atakuwa anapokea mshahara wa takriban shilingi milioni 306.7 kwa siku, milioni 12.78 kwa saa na Ksh 212,986 kwa dakika moja.