Kijana wa miaka 22 kutoka Wilaya ya Sheema nchini Uganda anadaiwa kumuua shabiki wa Arsenal kufuatia kutofautiana kuhusu mechi ya Ligi Kuu ya Uingereza kati ya Arsenal na Man United siku ya Jumapili.
Kulingana na Citizen Digital Kwa mujibu wa polisi, Jackson Aineruhanga aliuawa muda mfupi baada ya ushindi wa Arsenal dhidi ya Man United.
Wapenzi hao wawili wa kandanda walizozana baada ya bao la mchezaji wa Manchester United Alejandro Garnacho kufutwa kwa sababu ya kuotea.
“Inadaiwa jioni baada ya mechi, washabiki hao wawili walizua kutoelewana walipokuwa wakitazama mechi. Wawili hao baadaye walienda kwenye baa na wakafukuzwa kwa kusababisha fujo, na hapo ndipo vita vilipozidi,” msemaji wa Polisi Marcial Tumusiime alisema akinukuliwa na gazeti la Monitor.
Kulingana na Tumusiime, mshukiwa huyo kwa sasa anafuatiliwa na polisi baada ya mwathiriwa anayedaiwa kumchoma na kitu chenye ncha kali kifuani kufariki.
Tumusiime anabainisha kuwa kuna uchunguzi unaendelea na sampuli zimekusanywa kwa ajili ya uchunguzi zaidi wa kitaalamu.
"Tulitembelea eneo la uhalifu na kukuta kipande cha fimbo kikiwa na madoa ya damu na viatu vya washukiwa," alisema.
Mwili wa mwathiriwa ulipelekwa katika Kituo cha Afya cha Kabwohe kwa uchunguzi wa maiti