Msichana alilia haki baada ya kumwagiwa maji moto

mwanafuzi wa chuo achomwa na maji na mpenzi wake kaunti ya kisii

Muhtasari

•Familia kulilia haki baada ya mpenzi wa mschana wao kumchoma uso


Maji moto mekoni
Maji moto mekoni
Image: BBC NEWS

Mwanafunzi mmoja wa mwaka wa pili chuoni analilia haki baada ya kuchomwa na maji moto na mtu anayedai kuwa mpenzi wake .

Mercy Momanyi anauguza majeraa katika hospitali moja kaunti ya Kisii alisma kuwa familia ya mshukiwa inataka aondoe kesi dhidi ya mshukiwa ili aweze kusaidiwa.

Mwanafunzi huyu na ambaye anauguza majeraha ya moto usoni na mikononi anasema kuwa amepitia uchungu mwingi. 

Mercy alisimulia kuwa mpenzi wake wa miaka miwili ni sababu ya kuteseka kwake, mwanafunzi huyu anasema kuwa akiwa na mpenzi wake walitofautiana na akampiga na alichukua hatua ya kwenda kumweleze mamake mshukiwa.

Mschana huyu anasema kuwa mpenziwe akuwa anataka Mercy amwambie mamake mzazi ndiposa alichukua maji na ambayo yalikuwa moto na kumrushia mwilini,Mercy na ambaye ni mwanafunzi wa mwaka wa pili katika chuo moja kiambu .

Kinachotatiza Mercy ni kuwa japo anazidi kupata nafuu familia ya mpenziwe inataka atupilie kesi yake ili waweze kumlipia pesa na ambazo anadahiwa kwenye Hosptali.

y anaelezea kuwa familia yake haina uwezo wa kifedha kulipa hospitali na baada ya kufuatilia familia ya kijana aliyemumwagia maji wanasisitiza tu lazima kesi ilifikishwa kwa polisi itupiliwe mbali.

Mwanaharakati mmoja katika kaunti ya kisii asema anasema kuwa mashukiwa lazima apatikane hata kama amejificha mkono wa sheria utamfikia ili Mercy apate hakik.

Kulingana na daktari anayemhudumia Mercy anazidi kupata nafuu na asilimia ya majeraha yake ni aslimia 10a.

Kamanda wa polisi kaunti ya kisii anasema uchunguzi unaendelea ili kujua kilichojiri ndiposa Mercy apate haki.