logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Wachaneni na hii dialogue-Raila aambiwa

Njiru alizungumza hayo baada ya Wakenya wengi kuanza kulalamikia Mamlaka ya Nishati

image
na Radio Jambo

Habari16 September 2023 - 07:01

Muhtasari


  • Njiru alisisitiza kwamba hastlas wamechoka na kwamba wako tayari kufanya lolote ambalo Raila Amollo Odinga atawaambia.
Gachagua amshambulia Odinga tena

Ndegwa Njiru ni Wakili wa Kenya wa Mahakama Kuu. Yeye ni wakili anayejulikana na Wakenya wengi kwa sababu amekuwa akiwakilisha wanasiasa wenye nguvu katika kesi mahakamani.

Ndegwa Njiru amewaambia viongozi wa Azimio La Umoja One Kenya Alliance wakiongozwa na Raila Amollo Odinga, Stephen Kalonzo Musyoka, Martha Karua, Jeremiah Kioni na Eugene Wamalwa kwamba wanapaswa kusitisha Mazungumzo ya Kitaifa na serikali ya Muungano wa Kenya Kwanza inayoongozwa na Rais William Samoei Ruto.

Njiru alisisitiza kwamba hastlas wamechoka na kwamba wako tayari kufanya lolote ambalo Raila Amollo Odinga atawaambia.

Njiru alizungumza hayo baada ya Wakenya wengi kuanza kulalamikia Mamlaka ya Nishati ya Petroli na Udhibiti EPRA kupandisha bei ya mafuta ya petroli kama vile Petroli, Dizeli na Taa jana.

"Wachaneni na hii DIALOGUE we hit the road running....ardhi imeiva kwa kukimbia...ardhi imeiva...imeiva hadi kiini...HUSTLERS are ready uwezo na nia.. @RailaOdinga@skmusyoka@MarthaKarua@HonKioni@EugeneLWamalwa,"Ndegwa aliandika.

Wakati uo huo viongozi wa Azimio wakiongozwa na Odinga walikutana na kufanya waandishi wa habari na kuionya serikali ya Ruto dhidi ya kuongeza bei ya petroli, Dizeli na Mafuta taa kila mwezi.

 

 

 

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved