logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Zanzibar: Kisiwa ambacho ukipoteza pesa tangazo linawekwa redioni hadi uzipate!

Kwa mujibu wa Makala hayo, Zanzibar ndicho kisiwa au sehemu ambayo inachukuliwa kuwa salama Zaidi

image
na Davis Ojiambo

Habari18 September 2023 - 07:04

Muhtasari


  • • Kuwaelekeza wageni waliopotea na ambao wanatafuta ramani si jambo gumu kwa wana Zanzibar.
Zanzibar.

Katika moja ya Makala ya kustaajabisha ambayo yamefanywa na BBC, kisiwa cha Zanzibar ni moja ya sehemu ambayo ukarimu ni wa viwango vya kupitiliza.

Kwa mujibu wa Makala hayo kwa njia ya video, mtu yeyote katika kisiwa cha Zanzibar akipoteza pesa au mali yake, basi moja kwa moja ta ngazo linawekwa redioni hadi pale kitu hicho kitakapopatikana.

“Aliibiwa mgeni na baadhi ya watu ambao sio waaminifu, mwizi huyo alifuatiliwa na kikapatikana kitu chake na akatafutwa na mwenyewe akapewa. Ndio maana mpaka kesho watu huko nje ya Zanzibar wanahamasishana huku ni sehemu salama,” mzee mmoja mkaazi wa Zanzibar alisema.

Kwa mujibu wa Makala hayo, Zanzibar ndicho kisiwa au sehemu ambayo inachukuliwa kuwa salama Zaidi duniani kwa ukarimu ambao wageni haswa watalii wanaooneshwa na wenyeji.

Kuwaelekeza wageni waliopotea na ambao wanatafuta ramani si jambo gumu kwa wana Zanzibar.

“Unajua Zanzibar ni tamaduni zetu na mila zetu, hata mimi toka niko mdogo tulifundishwa kuwa wapole na wakarimu kwa watu tunaokutana nao. Na haswa haswa watu ambao hatuwajui. Kwa sababu huwezi kujua yule mtu usiyemjua ni nani, na hilo limekuwa jambo la kipekee linalofaya Zanzibar kuwa kivutio kwa watalii,” Nahya Zahir, mkaazi wa Zanzibar alisema.

Mzee Khatibu Mwinyi, mkazi wa Zanzibar aliiambia BBC kwamba ukarimu ni historia ya Zanzibar tangu kitambo akisema kuwa Imani ndio imewajenga wengi kuwa na ukarimu huo uliopitiliza.

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved