Mwanaume mmoja aliyejulikana kama Stoneman Willie atazikwa mazishi ya kawaida baada ya kuwekwa kwenye maonyesho katika nyumba ya mazishi iliyopo Reading, Pennsylvania nchini Marekani, kwa miaka 128.
Mtu huyo asiyejulikana alikuwa mlevi ambaye alikufa baada ya kuugua figo gerezani mnamo Novemba 19, 1895.
Mwili wake ulihifadhiwa kwa kuzungushwa ndani ya kipande cha nguo (mbinu ya kale iliyotumiwa kuhifadhi maiti hasa katika nchi ya Misri -ikijulikana kama Mummyification) kwa bahati mbaya na mtaalamu wa maiti anayejaribu mbinu mpya za kuhifadhi miili (zinazowafanya wafu wawe na muonekano wa mtu aliye hai kwa kuingiza kimiminika maalumu mwilini mwao (new embalming techniques), kulingana na Nyumba ya Mazishi ya Auman.
Akiwa amevalia suti nyeusi mtu huyo anaonyeshwa kwenye jeneza huku akiwa na kitambaa kingine chekundu kifuani mwake. Nywele na meno yake vimeendelea kuwa sawa, na ngozi yake imechukua muonekano wa ngozi.
Kwa sababu mtu huyo alitoa jina bandia wakati alipokamatwa kwa wizi wa mifuko, utambulisho wa Stoneman Willie haukujulikana kwa miaka mingi na maafisa wa eneo hilo hawakuweza kuwapata jamaa zake.
Nyumba ya mazishi ilikuwa imeomba serikali ruhusa ya kuuhifadhi mwili huo badala ya kuuzika ili kufuatilia mchakato wa majaribio ya kuaga mwili huo.
Lakini nyumba ya mazishi ya Auman inasema sasa imemtambua Stoneman Willie kwa kutumia nyaraka za kihistoria na itafichua jina lake baadaye wiki hii wakati watakapouzika mwili huo.
Hadi sasa, hakuna mengi yaliyojulikana juu yake zaidi ya mizizi yake kuwa ni taifa la Ireland.