logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Polisi wamkamata mwanamke aliyemdunga mumewe kisu hadi kufa Kisii

Alimchoma kisu mara kadhaa shingoni na kichwani akimuacha kwenye dimbwi la damu.

image
na Radio Jambo

Habari04 October 2023 - 11:02

Muhtasari


  • Mshukiwa, 35 alinaswa Jumanne jioni kutoka kwa nyumba ya jamaa Kayole jijini Nairobi alikokimbilia.

Maafisa wa upelelezi kutoka Kisii mnamo Jumatano walisema walimkamata mwanamke anayeshukiwa kumuua mumewe ambaye walitengana naye katika eneo la Jogoo Jumatatu usiku.

Mshukiwa, 35 alinaswa Jumanne jioni kutoka kwa nyumba ya jamaa Kayole jijini Nairobi alikokimbilia.

Mwanamke huyo anashukiwa kuvamia nyumba ya kupanga eneo la Jogoo huko Kisii Jumatatu usiku ambapo marehemu, 45, aliishi na mpenzi wake, ambaye pia ni mwanafunzi wa chuo kikuu.

Alimchoma kisu mara kadhaa shingoni na kichwani akimuacha kwenye dimbwi la damu.

Alifariki saa chache baadaye huku madaktari wakimhudumia katika Hospitali ya Kufundisha na Rufaa ya Kisii.

Kamanda wa polisi wa kituo cha polisi cha Kisii Central Amos Ambasa alisema mshukiwa atafikishwa mahakamani kujibu mashtaka ya mauaji.

"Tayari yuko njiani kuja hapa na atafikishwa mahakamani," aliambia Radiojambo Jumatano.

 

 

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved