logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Wabunge wa Zimbabwe wapoteza viti kwa sababu ya barua bandia

Barua ilitiwa saini na "Sengezo Tshabangu",aliyedai kuwa katibu mkuu wa CCC.

image
na Davis Ojiambo

Habari11 October 2023 - 09:31

Muhtasari


  • • Barua ya Jumatatu ilitiwa saini na "Sengezo Tshabangu", ambaye alidai kuwa katibu mkuu wa Citizens Coalition for Change (CCC).

Wabunge 15 wa upinzani nchini Zimbabwe wamewasilisha rufaa mahakamani wakisema walidanganywa ili kupoteza viti vyao vya ubunge.

Hii imekuja baada ya mtu mmoja aliyedai kuwa Katibu wa chama hicho kwa uongo kusema kuwa wabunge hao si wanachama tena.

Alipopokea barua hiyo ya ulaghai, spika wa bunge la Zimbabwe alitangaza kuwa viti 15 viko wazi.

Matokeo ya uchaguzi mdogo yanaweza kukabidhi chama tawala cha Zanu-PF idadi kubwa inayohitaji kufanya marekebisho ya katiba.

Barua ya Jumatatu ilitiwa saini na "Sengezo Tshabangu", ambaye alidai kuwa katibu mkuu wa Citizens Coalition for Change (CCC), chama kikuu cha upinzani nchini Zimbabwe.

Ilikuwa imejaa makosa ya kisarufi.

Kiongozi wa CCC Nelson Chamisa alimtaka spika Jacob Mudenda kupuuza barua hiyo akisema chama hicho hakina katibu mkuu na hakijamfukuza wala kumrudisha mbunge yeyote.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved