Jambazi aliyekuwa akisakwa alipigwa risasi na kuuawa katika makabiliano na polisi huko Kehancha, kaunti ya Migori.
Polisi walisema walipata bunduki ya kujitengenezea ikiwa na risasi 13 kutoka kwa jambazi huyo, huku wenzake wawili wakifanikiwa kutoroka.
Kwa mujibu wa polisi,washukiwa hao walikuwa wanasakwa kwa kuhusika na wizi wa mabavu pamoja na mauaji eneo la Kuria, Magharibi.
Walisema kuwa, kundi la watu lilishambulia nyumba ambayo jamaa huyo alikua amejificha na kusababisha mashambuliaji ya risasi kabla ya jambazi huyo kuangushwa.
Aidha polisi wathibitisha kuwa jamaa wawili waliokuwa pamoja na jambazi huyo walifaulu kutoroka,huku wakianzisha uchunguzi dhidi yao zikianzishwa.
Hata hivyo,maafisa wa polisi walianikiwa kunasa silaha na bidhaa zingine ambazo walisema zinatumiwa kutekeleza maovu kwenye maeneo hayo.
Bunduki moja ambayo polisi walisema ni ya kujitengenezea, risasi 13, cartridge moja, pikipiki moja na zilipatikana kutoka kwa mshukiwa hao wa majambazi.
Mwili wa mshukiwa ulihamishwa hadi kwenye chumba cha kuhifadhia maiti ukisubiri kufanyiwa uchunguzi.
Kisa hiki cha wizi wa mabavu si cha kwanza kuripotiwa,kwani watu wamekuwa wakiangaisha wakaaji wa eneo hilo na kuib mali na hata hela kutoka kwao.
Huko Masaba, Kehancha, polisi walisema genge moja lilivamia boma moja na kuwaacha wakazi kukadiria hasara ya takriban Sh50,000.