Saa chache baada ya mahakama kutupilia mbali kesi dhidi ya mhubiri Ezekiel Odero alimshukuru Muumba wake kwa kuwa mwaminifu ndani ya maisha yake baada ya kutopatikana na kosa kwa kesi iliyomkumba.
Kiongozi huyu wa Kanisa alitoa kauli hii baada ya kuandaa ibada ya kuwaombea wafuasi wake wanaofuatilia mahubiri yake kwenye Runinga na mitandao ya kijamii.
"Mungu ni mwaminifu kwa mja wake ,hakika ameniondolea huofu wote na kusafisha Jina langu kupitia kanisa lake,nilipitia Mengi, kanisa likafugwa kwa siku chache,mahubiri yangu kwenye Runinga yakakatizwa kwa muda,"alisema.
Mchungaji huyu alisimulia jinsi kongamano za moambi alizoweka kwa kaunti tofauti zilikatizwa licha ya kuwa alikuwa amezigharamikia.
"Wakati ufika kwa maisha ya mwanadamu jina litapakwa tope ila Mungu ni mwaokozi wa wote wanaomtumaina mapito haya yalikuwa sehumu Mungu kuonesha upendo wake kwa kanisa lake,"alisema Ezekiel.
Kiongozi huyu wa kanisa la New Life Prayer Center Mavueni alionesha ushaidi wa cheti cha korti alichopewa kwa wafuasi wake akishukuru maafasi wa kitengo cha kupambana na ufisadi kwa kukamilisha uchunguzi wao kwa haraka na Korti kumuachiliia Huru.
Ezekiel Odero alishtakiwa kortini kwa shutma za kuwa na urafiki na mchungaji mwenye utata Paul Mackenzie aliyedaiwa kuhusika na vifo vya watu zaidi ya 45O kesi ambayo ilikosa ushaidi na kutupliwa mbali na mahakama.
Mchungaji huyu pia alikesiwa kuwa na makavani ndani ya kanisa lake jambo ambalo lilichuguzwa na kamati ya seneti na kubaini kuwa kilikuwa chumba cha kusambaza umeme.