Hafla ya 67 ya Ballon d’Or ilifanyika usiku wa Jumatatu, Oktoba 30 kwenye ukumbi wa Théâtre du Châtelet jijini Paris, Ufaransa ambapo kulikuwa na washindi tofauti katika vipengele mbalimbali.
Staa wa soka wa Argentina, Lionel Messi alishinda taji la Ballon d’Or kwa Wanaume kwa mara ya nane katika maisha yake ya soka baada ya kupata mafanikio makubwa katika mwaka mmoja uliopita.
Kiungo wa kati wa timu ya wanawake ya Barcelona, Aitana Bonmati kwa upande mwingine alishinda Tuzo ya Ballon d’Or ya Wanawake 2023, ikiwa ni mara ya kwanza kwa Mhispania huyo kushinda taji hilo la kifahari.
Manchester City ilishinda tuzo ya klabu bora ya mwaka wa 2023 ya Wanaume huku Barcelona Women ilishinda Klabu ya Wanawake ya mwaka.