logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mwanaume raia wa Ghana akamatwa akiwa na risasi JKIA akielekea Dubai

Polisi walisema kuwa mshukiwa amekaa jijini Nairobi kwa muda.

image
na Davis Ojiambo

Habari03 November 2023 - 14:30

Muhtasari


  • •Alihojiwa na baadaye kukabidhiwa kwa Kitengo cha Polisi cha Kupambana na Ugaidi kwa maelezo zaidi.
  • •Mwanamume huyo alitarajiwa kortini ambapo polisi walipanga kuomba muda zaidi wa kumshikilia huku wakichunguza tukio hilo.
  •  

Kulishuhudiwa kizazaa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta wakati mwanamume raia wa Ghana aliyekuwa safarini kwenda Dubai alipokamatwa akiwa amebeba risasi tatu.

Polisi walisema mwanamume huyo mwenye umri wa miaka 33, alinaswa katika eneo la uchunguzi wa uwanja wa ndege alipokuwa akipanga kuondoka kwa ndege ya shirika la ndege la Kenya Airways.

Raia huyu alipatikana na risasi  hizo kwenye kituo hicho ambapo ni kinyume cha  sheria  katika tukio la Jumatano, polisi walisema.

Polisi walisema alinyimwa kuondoka, akahojiwa na baadaye kukabidhiwa kwa Kitengo cha Polisi cha Kupambana na Ugaidi kwa maelezo zaidi.

Nia yake ya kumiliki risasi hizo na kujaribu kusafiri  nazo hadi Dubai bado haijafichuliwa.

Mwanaume huyu alibainika kuwa alikuwa amekaa  jijini Nairobi kwa muda, polisi wakibaini kuwa wanashuku kuwa alitoka na risasi hizo nchini. 

"Uchunguzi unaendelea kubaini chanzo cha risasi hizo," polisi walisema.

Mwanamume huyo alitarajiwa kortini ambapo polisi walipanga kuomba muda zaidi wa kumshikilia huku wakichunguza tukio hilo.

Risasi ni miongoni mwa vitu vilivyopigwa marufuku kwenye ndege. Abiria wanatakiwa kuzisalimisha kwa mashirika ya ndege na kutoa hati za kuzimiliki.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved