logo

NOW ON AIR

Listen in Live

YouTuber wa Marekani, Mr Beast apongezwa kuchimba visima 52 vya maji Kenya

Akiwa nchini, alijenga  daraja  lililokuwa katika hali mbaya hasa wakati huu wa mvua ya masika.

image
na Davis Ojiambo

Habari06 November 2023 - 07:29

Muhtasari


  • • YouTuber huyo alianza kazi ya kuchimba visima 100 barani Afrika huku 52 vikiwa nchini Kenya.
  • • Kulingana na yeye alishtushwa na maji machafu ambayo watoto hutumia wakiwa shuleni.
  • • "Visima hivi 100 tulivyojenga barani Afrika vitabadilisha maisha mengi lakini kwa hakika haitoshi. Ndiyo maana tunahitaji msaada wako," 
JIMMY DONALDSON MWANA YOUTUBA WA MAREKANI

Wakenya wamewakosoa viongozi katika utoaji huduma za serikali baada ya YouTuber wa  Marekani Jimmy Donaldson almaarufu Mr Beast kuchimba mabwawa 52 nchini.

YouTuber huyo alianza kazi ya kuchimba visima 100 barani Afrika huku 52 vikiwa nchini Kenya. Kulingana na yeye alishtushwa na maji machafu ambayo watoto hutumia wakiwa shuleni.

Kulingana na muundaji wa maudhui, miradi kama hiyo haihitaji pesa nyingi kutoka kwa serikali, ila tu watu wenye nia njema ya kusaidia.

Aliwataka wananchi wenye nia njema  kuendelea kuchangia fedha ili kusaidia ujenzi wa visima vingi na kufanya miradi mingi ya kuboresha maisha ya binadamu.

"Visima hivi 100 tulivyojenga barani Afrika vitabadilisha maisha mengi lakini kwa hakika haitoshi. Ndiyo maana tunahitaji msaada wako," alisema.

Kisima kinapochimbwa, maji huhamishiwa kwenye matangi yaliyo kwenye minara ya maji ili kutoa maji safi na yanayofikika kwa urahisi kwa wenyeji.

Donaldson alifichua kuwa mradi huo wa bara ulichukua zaidi ya miezi minane kukamilika

Mtayarishaji maudhui aliye na zaidi ya watu milioni 200 waliojisajili kwenye YouTube alishiriki safari inayoonyesha kabla na baada ya miradi.

Akiwa nchini, alijenga  daraja  lililokuwa katika hali mbaya hasa wakati huu wa mvua ya masika.

Pia alitoa kompyuta, rafu, vitabu, vifaa vya kucheza, ubao mweupe na projekta kwa shule za msingi nchini.

Pia alikwenda Zimbabwe, na Cameroon kujenga visima zaidi ili kubadilisha maisha ya wenyeji.

Wakizungumzia suala hilo, Wakenya walichukua fursa hiyo kulinganisha miradi ya Bw Beast na ile iliyoanzishwa na viongozi wa humu nchini.

Baadhi ya Wakenya walilalamika kwambaviongozi hutumia rasilimali nyingi zaidi kuzindua miradi badala ya jumla ya pesa zinazotumiwa katika miradi yenyewe.

Pia walielezea hofu kwamba baadhi ya viongozi wa eneo hilo wanaweza kuchukua sifa kwa miradi ya Donaldson.

“Tuangalie viongozi kwa makini, wanaweza kwenda kuzindua hivi visima,” mmoja alitoa maoni yake.

Wengine walikumbuka kisa cha Waziri wa Mambo ya Ndani Kithure Kindiki alipokuwa Seneta wa Tharaka Nithi alipozindua darasa la udongo baada ya kuwasili kwa chopa.

"Bw Beast amefanya kile ambacho viongozi wetu walipaswa kufanya zamani. Kenya pekee inalia kuhusu uhaba wa maji ilhali kuna suluhu," Mkenya mmoja alisema.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved