Serikali kupitia kwa wizara ya usalama wa ndani imetangaza Jumatatu Novemba 13 kama sikukuu ya upanzi wa miti kote nchini.
Tangazo hili lilichapishwa katika gazeti rasmi la serikali ya waziri Profesa Kithure Kindiki ambaye alisema ni vyema kwa Kenya kutumia vizuri fursa ya mvua za masika ya El Nino kupanda miti kama njia moja ya kuafikia azimio la serikali ya Kenya Kwanza.
Katika notisi ya gazeti la serikali ya Novemba 6, Prof Kindiki alisema Rais William Ruto ataongoza nchi katika zoezi la ukuzaji miti kuambatana na mpango kabambe wa utawala wake wa kukuza miti bilioni 10 kufikia 2032.
"Katika kutekeleza mamlaka yaliyotolewa na kifungu cha 3 cha Sheria ya Likizo ya Umma, Katibu wa Baraza la Mawaziri wa Mambo ya Ndani na Utawala wa Kitaifa anatangaza Jumatatu, Novemba 13, 2023, sikukuu ya umma ambayo umma utashiriki katika ukuaji wa miti nchini kote," inasomeka. taarifa kwa sehemu.
"Zoezi hili ni sehemu ya Mpango wa Kurejesha Mazingira na Mazingira nchini Kenya–Kuelekea Ukuzaji wa miti bilioni kumi na tano (15). Kutakuwa na ukumbi maalum wa Kitaifa wa upandaji miti utakaoongozwa na Mheshimiwa (Dkt.) William Samoei Ruto."
Zoezi la upandaji miti pia litaangaziwa katika kaunti 47 zikisimamiwa na Mawaziri na Magavana, ambapo raia wote wa Kenya na umma kwa jumla watatarajiwa kushiriki.
Hatua ya kutangaza Novemba 13 kuwa sikukuu ya umma inafuatia uamuzi wa Baraza la Mawaziri lililoketi Mombasa mnamo Ijumaa, Novemba 3, 2023 kuhusu hitaji la kuokoa nchi kutokana na athari mbaya za Mabadiliko ya Tabianchi.
Wakati huo huo, mitihani ya kitaifa iliyopangwa kwa siku hiyo itaendelea kama kawaida.