logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Siwezi kukaa chini kusikiza uongo, Seneta Edwin Sifuna

Rais William Ruto kutarajiwa kuhutubia mabunge yote leo

image
na Davis Ojiambo

Habari09 November 2023 - 10:31

Muhtasari


  • •Haya yanajiri saa chache baada ya mkutano wa Rais kuhutubia kikao cha pamoja cha Bunge la Kitaifa na Seneti Alhamisi alasiri.

Katibu mkuu wa chama cha ODM ambaye pia ni Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna kupitia mtandao wake wa X,ameeleza kwanini hatahudhuria Kikao cha hotuba ya Rais William Ruto hivi leo.

Kulingana na seneta huyu kwenye taarifa alisema kuwa Rais William Ruto ameshidwa kuonesha picha nzuri katika uongozi wake wakati huu hali ya uchumi katika taifa inaadhirika.

"Ruto hawezi kuaminiwa kutoa picha halisi ya hali ya taifa ambayo unajua ni mbaya,"ilisema taarifa hiyo.

Katibu huyu wa ODM alitoa kauli ya pili kwenye mtandao wake akisema kuwa kuudhuria mkutano huyo hawezi kwani akuna jambo la ukweli litahafikiwa.

"Siwezi kukaa chini na kusikiliza uwongo,"ilisema hivo taarifa hiyo.

Haya yanajiri saa chache baada ya mkutano wa Rais kuhutubia kikao cha pamoja cha Bunge la Kitaifa na Seneti Alhamisi alasiri.

Maspika kutoka mabunge yote mawili, Moses Wetang'ula (Bunge la Kitaifa) na Amason Kingi (Seneti) walikuwa wametoa wito kwa wanachama wote kujitokeza katika majengo ya Bunge.

Hotuba hiyo itakuja miezi 14 baada ya Ruto kuwa Rais wa tano wa Kenya. Hotuba ya mwisho ya Hali ya Kitaifa ilitolewa na aliyekuwa Rais Uhuru Kenyatta mnamo Novemba 30, 2021.​

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved