Makachero wa DCI katika kaunti ya Kisii wamemdaka mwanamume mmoja anayeshukiwa kuwaua watoto na mke wa ndugu yake.
Kwa mujibu wa taarifa ambayo ilichapishwa kwenye kurasa za mitandao ya kijamii za DCI, mwanamume huyo mwenye umri wa miaka 27, Alex Ayata Migosi kutoka kijiji cha Mesaria kaunti ya Kisii alikamatwa baada ya kuchimba mitini kufuatia tukio hilo la unyama.
“Alex Ayata Migosi ambaye alikimbilia mafichoni baada ya mauaji hayo kunaswa jana usiku, saa chache baada ya kisa cha Jumanne tarehe 14 eneo la Kegogi katika kaunti ndogo ya Marani, Kisii,” sehemu ya taarifa ya DCI ilisom.
DCI walisema kwamba muda mfupi kabla ya tukio hilo, majirani waliripotiwa kushuhudia makabiliano makali kati ya mshukiwa wa mauaji na kakake Patrick Omuga kuhusu suala ambalo halijathibitishwa.
Katika azimio la kuchukiza la kusuluhisha matokeo, Ayata aliingia kisiri ndani ya nyumba ya ndugu huyo akiwa na panga, akiwaua kwa uchungu wale watatu waliokuwa wanyonge kwa hofu na shutuma za ujirani.
Vikosi vya usalama vya eneo hilo vilihamasishwa kumzuia mhalifu huyo kabla hajaondoka mkoani humo, juhudi ambazo zilizaa matunda jana usiku.
Kwa sasa anashughulikiwa ili afikishwe mahakamani.
Aliwaua mke wa ndugu yake pamoja na watoto wawili wenye miaka 4 na 3 mtawalia.