logo

NOW ON AIR

Listen in Live

KCPE 2023: Mtahiniwa bora apata alama 428

Mitihani ya mwaka huu ilikuwa na watahiniwa milioni 1.4.

image
na Samuel Maina

Habari23 November 2023 - 08:11

Muhtasari


  • •Alhamisi asubuhi, Waziri wa Elimu Ezekiel Machogu alitangaza kwamba ni watahiniwa 8,523 pekee waliopata zaidi ya alama 400.
wakati wa kuchapishwa kwa matokeo ya mtihani wa KCPE wa 2023 katika jumba jipya la KNEC Mitihani House mnamo Novemba.

Mtahiniwa bora zaidi wa Mtihani wa Kitaifa wa Darasa la Nane (KCPE) 2023 alipata alama 428 kati ya 500.

Mnamo Alhamisi asubuhi, Waziri wa Elimu Ezekiel Machogu alitangaza kwamba ni watahiniwa 8,523 pekee waliopata zaidi ya alama 400.

“Idadi ya watahiniwa ambao walipata alama 400 hadi 500 ilikuwa 8,525 ambayo ni sawa na asilimia 0.60,” Waziri Machogu alisema.

Waliopata alama kati ya 300 hadi 399 walikuwa 352,782 ambayo ilikuwa 24.29%.

“Alama 200 hadi 299, watahiniwa waliokuwa katika kundi hilo walikuwa 658,278, ambayo ni asilimia 48.49,” alisema Machogu.

Waliopata kati ya alama 100 hadi 199 walikuwa 383,025, huku waliopata kati ya alama 0 hadi 99 walikuwa watahiniwa 2,060.

Mitihani ya mwaka huu ulikuwa na watahiniwa milioni 1,406,557.

Watahiniwa, wazazi wao na walezi sasa wanaweza kupata matokeo kupitia tovuti ya Baraza la Kitaifa la Mitihani la Kenya (KNEC), mfumo wa SMS ama katika afisi za elimu za kaunti na shule zao.

Kwa chaguo la SMS, watahiniwa wanapaswa kutuma nambari yao ya usajili (index number), ikifuatiwa na neno KCPE (katika herufi kubwa)  kwa 40054 ili kupata matokeo.

"Wazazi na watahiniwa wanaweza kupata matokeo yao ya KCPE kwa kutuma nambari zao za usajili kwa nambari 40054. SMS hiyo itatozwa Sh25," Waziri Machogu alisema.

Mfumo wa SMS unapatikana kwa huduma zote za simu na itatozwa Sh25 kila moja.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved