Jumuiya ya Afrika Mashariki imekubali ombi la Somalia kujiunga na jumuiya hiyo, ambapo mkataba wa kukubaliwa unatarajiwa kutiwa saini hivi karibuni.
Hayo yalisemwa jana na mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) anayeondoka Rais wa Burundi, Everiste Ndayishimiye.
Bw Ndayishimiye pia amesema kuwa kikao cha marais kimekubaliana kwamba wakuu wa majeshi ya EAC wanatarajiwa kufanya kikao cha kutathmini hatua itakayochukuliwa kwa kikosi cha kanda hiyo (EACR) kilichoombwa kuondoka mwishoni mwa mwaka huu.
Katika kikao cha leo, rais wa Somalia Hassan Sheikh alipokelewa rasmi katika jumuiya na katibu mkuu Peter Mathuki, ambapo mkataba ukishatiwa saini Somalia inakuwa mwanachama wa nane baada ya Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) kujiunga mwaka wa 2022.
Kikao cha faragha cha marais kilichofanyika mapema Ijumaa, kimekubaliana pia kuhusu mkutano wa michango ambayo kila mwanachama anatarajiwa kutoa ili kuboresha shughuli za jumuiya.
Katika kikao cha leo, Rais Salva Kiir anakabidhiwa uenyekiti wa EAC.
Marais wanaohudhruia, ni Mwenyeji Samia Suluhu wa Tanzania, william Ruto wa Kenya, Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda, Hassan sheikh wa Somalia ambaye ni mgeni maalum, Salva Kiir wa Sudan Kusini, na Evereste Ndayishimie wa Burundi.
Marais wa Rwanda na DRC wamewakilisha na wajumbe maalum wa marais wan chi hizo.