Mji wa kusini wa Gaza wa Khan Younis, mojawapo ya maeneo makuu ya mapigano ya sasa umeshambuliwa kwa mabomu.
Israel ilisema siku ya Jumatano kuwa vikosi vyake vinazingira eneo hilo.
Siku ya Alhamisi ilisema kuwa "imewaua magaidi wa Hamas na kushambulia maeneo kadhaa ya ugaidi" katika mji huo.
Picha kutoka jiji hilo kupitia mashirika ya Habari,nyingi zinahuzunisha sana ikiwa ni pamoja na matukio ya watu waliojeruhiwa wakipelekwa hospitalini, na wengine wakiwa wamelala kwenye sakafu iliyojaa watu wakisubiri matibabu - pamoja na wanawake na watoto wadogo miongoni mwao.
Hizi hapa ni picha chache tu za yanayojiri katika jiji hilo.
Onyo: Unaweza kuona baadhi kuwa za kuhuzunisha.