logo

NOW ON AIR

Listen in Live

DCI wafichua jinsi muuaji wa Starlet Wahu amekuwa akiendesha shughuli zake

DCI walisema Matara anashukiwa kuwa mnyanyasaji wa kimapenzi anayeweza kuwa sehemu ya genge linalolenga wanawake kwenye tovuti za uchumba.

image
na Samuel Maina

Habari08 January 2024 - 04:50

Muhtasari


  • •DCI ilithibitisha kuwa mshukiwa John Matara kwa sasa yuko mikononi mwa polisi na uchunguzi wa mauaji hayo unaendelea.
  • •DCI walisema Matara anashukiwa kuwa mnyanyasaji wa kimapenzi anayeweza kuwa sehemu ya genge linalolenga wanawake kwenye tovuti za uchumba.
Starlet Wahu, dadake Pasta Kanyari

Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) imetoa taarifa kuhusu uchunguzi unaoendelea wa mauaji ya mwanasosholaiti wa Kenya, Starlet Wahu.

Mwili wa marehemu Wahu uligunduliwa siku ya Alhamisi asubuhi katika chumba cha ghorofa ya nne cha AirBnB ya Papino Apartments kilichoko katika mtaa wa South B katika Jiji la Nairobi. Hii ilikuwa baada ya mlinzi kuripoti kumuona mshukiwa, John Matara, akikimbia eneo la tukio.

Katika taarifa yao ya Jumapili jioni, DCI ilithibitisha kuwa mshukiwa huyo mwenye umri wa miaka 34 kwa sasa yuko mikononi mwa polisi na uchunguzi wa mauaji hayo unaendelea. Wapelelezi pia waliwasihi manusura wengine wa chuki ya mshukiwa kujitokeza na kuripoti masaibu yao.

"Wakati uchunguzi wa mauaji ya kinyama ya mwanasosholaiti Starlet Wahu Mwangi mwenye umri wa miaka 26 ukiendelea huku mshukiwa mkuu John Matara akiwa chini ya ulinzi wa polisi, DCI inawaomba waathiriwa na manusura wa uhasama wa mshukiwa kuripoti masaibu yao katika Ofisi ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai ya Eneo la Nairobi au kituo cha polisi cha karibu,” DCI ilisema kwenye taarifa.

DCI iliripoti kuwa Matara alizuiliwa katika Kituo cha Polisi cha Industrial Area baada ya kukamatwa katika Hospitali ya Mbagathi jijini Nairobi ambapo alikuwa akitafuta matibabu kutokana na majeraha kidogo ya mkono na mguu. Alikamatwa pamoja na rafiki yake wa miaka 25, Anthony Nyongesa ambaye alikuwa akimsaidia hospitalini.

Wapelelezi walidai kuwa mshukiwa huyo ni mnyanyasaji wa kimapenzi ambaye anaweza kuwa sehemu ya genge linalolenga wanawake kwenye tovuti za uchumba.

"Uchunguzi kwa sasa unaelekeza kwa uwezekano wa mkosaji wa kingono ambaye hufanikiwa kwa kuwahadaa waathiriwa wake, na ambaye anaweza kuwa sehemu ya wahalifu wanaolenga wanawake kwenye tovuti za uchumba na Programu zingine za mitandao ya kijamii," DCI ilisema.

Waliongeza, "Tunapopongeza wale ambao wamechukua hatua ya ujasiri ya kuripoti matukio yao mabaya na Matara na/au wanachama wa genge lake linaloshukiwa, tunawahimiza mashahidi zaidi wa ukatili na mashambulizi ya kutisha kujitokeza na kurekodi taarifa na wapelelezi wetu. .”

Makachero hao pia walithibitisha kujitolea kwao kuchunguza mauaji ya dadake kasisi maarufu Victor Kanyari mwenye umri wa miaka 26.

Sambamba na hayo, waliwataka wananchi kujihadhari na wahalifu kama John Matara wanaojifanya wapenzi lakini wanawageukia wale wanaoingia kwenye mtego wao.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved