Maajabu! Fahamu kwa nini jamaa huyu aliajiri watu kumkata sehemu zake za siri

Damien Byrnes, 36, aliondoa uume na korodani za Marius Gustavson kwa kisu Februari 2017.

Muhtasari

•Byrnes, pamoja na Jacob Crimi-Appleby, 23, na Nathaniel Arnold, 48, walikiri kosa la kudhuru mwili kwa makusudi.

•Naye Gustavson alikiri makosa ya kula njama ya kufanya madhara mabaya ya mwili wake, na atahukumiwa mwezi Machi.

alikiri kosa la kutoa sehemu za siri za Marius Gustafson ingawa aliombwa na mwenyewe kufanya hivyo
Damien Byrnes alikiri kosa la kutoa sehemu za siri za Marius Gustafson ingawa aliombwa na mwenyewe kufanya hivyo
Image: BBC

Mwanaume mmoja ambaye aliajiriwa ili kukata sehemu za siri za mwanaume aliyekubali mwenyewe na kurekodi tukio hilo katika mtandao wa pay-per-view amefungwa jela miaka mitano.

Damien Byrnes, 36, aliondoa uume na korodani za Marius Gustavson kwa kisu Februari 2017.

Byrnes, pamoja na Jacob Crimi-Appleby, 23, na Nathaniel Arnold, 48, walikiri kosa la kudhuru mwili kwa makusudi.

Crimi-Appleby aliuweka mguu ya Gustavson kwenye barafu, na kusababisha kukatwa, huku Arnold akikata sehemu ya chuchu ya Gustavson.

Crimi-Appleby amefungwa jela miaka mitatu na miezi minane. Arnold amehukumiwa kifungo cha miaka miwili jela.

Mahakama ya Old Bailey ilielezwa kuwa tukio lililofanywa na Byrnes linahusishwa na utamaduni ambao wanaume hukubali kuondolewa sehemu zao za siri – kwa kukatwa uume na korodani.

Mwendesha mashtaka Caroline Carberry KC alisema Byrnes, kutoka Tottenham kaskazini mwa London, alikuwa miongoni mwa watu 10 walioshtakiwa kwa kushiriki katika tukio hilo.

Carberry alieleza mahakamani kwamba Byrnes aliajiriwa na Gustavson, ambaye amehusika mara kadhaa kuondoa sehemu za siri za wanaume wengine.

Tukio Lenyewe

Polisi wanasema hiki ni kisu ambacho Byrnes alikitumia kumkata Gustafson uume na korodani.
Image: BBC

Naye Gustavson alikiri makosa ya kula njama ya kufanya madhara mabaya ya mwili wake, na atahukumiwa mwezi Machi.

Bi Carberry alisema mahakama kuwa Disemba 2016 Byrnes "alikubali" kumkata viungo Gustavson kwa pauni 500 akijua kwamba tukio hilo litarikodiwa, lakini Gustavson alipunguza malipo hadi pauni 50.

Kabla ya tukio hilo, Byrnes alimwambia Gustavson: "Sina tatizo kufanya hivyo, lakini si utapoteza damu nyingi, karibu kufa?"

Lakini Gustavson aliwambia Byrnes kwamba atachoma na kufungwa kamba na kisha atamuelekeza Byrnes nini cha kufanya, mahakama ilielezwa.

Video ya kutisha ya ukeketaji wa viungo vya siri haikuonyeshwa mahakamani lakini ilielezewa na Bi Carberry, ambaye pia alisema baada ya Byrnes kuondoka, Gustavson alipiga simu polisi.

Utetezi wa Crimi-Applesby ulitokana na ukweli kwamba Gustafson "alimshawishi"
Image: BBC

Korti ilielezwa kwamba Gustavson alitibiwa hospitalini na kuruhusiwa baada ya siku kadhaa na akapewa rufaa kwa ajili ya uchunguzi wa akili.

Byrnes hakupokea malipo na alitishia kwenda polisi, mahakama ilielezwa, lakini Gustavson alijibu kwa kusema atamripoti kwa kumtishia, kumchafua na ukeketaji.

Baadaye kwa muda wa miaka miwili, Gustavson alimlipa Byrnes zaidi ya pauni 1,500.

Crimi-Appleby, 23, kutoka Epsom, Surrey, alikiri kuugandisha mguu wa Gustavson kwenye barafu, Februari 2019.

Wakati wa kesi hiyo, mahakama ilionyeshwa video ya mguu wa Gustavson ukiwa kwenye ndoo ya barafu kavu, huku Crimi-Appleby ikiongeza barafu zaidi.

Gustavson, ambaye sasa anatumia kiti cha magurudumu, alipokea takribani pauni 18,000 kama malipo ya faida, mahakama ilielezwa.

Nathan Arnold, muuguzi mwenye umri wa miaka 48 kutoka Kensington, Kusini magharibi mwa London, alikiri kukata moja ya chuchu za Gustavson, mwaka 2019.

Pia, alikiri kosa la wizi wa kuiba dawa ya ganzi kati ya 2016 na 2022 katika Hospitali ya Chelsea na Westminster, ambako alikuwa akifanya kazi.

Baada ya kukamatwa 2022, Byrnes alikiri alichofanya na kusema alikuwa na shida ya kifedha na alitapika baada ya kukata sehemu za siri za Gustavson.

Idhini sio utetezi

Wakili wa Arnold alisema mteja wake alikuwa muuguzi "mwenye huruma na mpole".
Image: BBC

Lisa Bald aliiambia mahakama mteja wake Byrnes "anajisikia aibu kwa kile alichokifanya.”

Wakili Neil Griffin alimuelezea Arnold kama muuguzi mwenye huruma, mpole, na mwenye heshima ambaye alitenda makosa hayo wakati akiwa hajielewi.

Sean Poulier alisema mteja wake Crimi-Appleby alishawishiwa na mtu mzima Gustavson baada ya kuingiA kwenye mtego wake.

Polisi walisema kama sehemu ya uchunguzi "walitazama saa kadhaa za picha hizo za kutisha na walisafiri kote Uingereza kutafuta waathiriwa na mashahidi, na waliwasiliana na vikosi vya polisi vya Uingereza na ng'ambo ili kuwafikisha watu hao mahakamani".

Kate Mulholland, Mwendesha wa London, alisema: "Idhini sio utetezi kwa upasuaji haramu ambao wanaume hao walishiriki kwa hiari kuondoa uume, mguu na chuchu katika mazingira hatarishi kwa maisha."