logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Pasta Kanyari akukutana ana kwa ana ndani ya korti na mshukiwa wa mauaji ya dadake (video)

Mahakama iliweka tarehe mpya, Februari 26 kama siku ya kutajwa tena kwa kesi hiyo.

image
na Davis Ojiambo

Habari04 February 2024 - 05:41

Muhtasari


  • • Mahakama iliweka tarehe mpya, Februari 26 kama siku ya kutajwa tena kwa kesi hiyo ili kubaini hatima ya John Matara. 
John Matara akutana uso kwa uso na pasta Kanyari, kakake Starlet Wahu.

Mchungaji Victor Kanyari kwa mara ya kwanza walikutana na mshukiwa mkuu katika mauaji ya dadake, Starlet Wahu, John Matara.

Kukutana kwao kwa hali ya ukakasi mwingi kulijiri katika mahakama ya Milimani Ijumaa ambapo Matara alikuwa anasomewa mashtaka ya mauaji ya mwanasosholaiti Wahu baada ya uchunguzi kukamilika.

Hata hivyo, Matara ambaye alionekana akiwa nadhifu kwa suto nyeusi na nywele zilizochanwa vizuri alikanusha mashtaka dhidi yake akijitetea kwamba yeye siye aliyesababisha kifo cha kikatili cha dadake pasta Kanyari.

Upande wa mashtaka wa serikali ulitaka mshukiwa azuiwe kupata uhuru kwa masharti ya dhamana. Wakati wote wa kesi hiyo, Matara aliyevalia nadhifu alionekana akiwa ameketi kwa wasiwasi huku shtaka likisomwa.

Katika video hiyo, kwa upande mwingine alionekana Pasta Kanyari ambaye alikuwa anafuatilia kwa umakini mkubwa kesi hiyo ikisomwa na waliangaliana na Matara ana kwa ana.

Mahakama iliweka tarehe mpya, Februari 26 kama siku ya kutajwa tena kwa kesi hiyo ili kubaini hatima ya John Matara.

Tazama video hii hapa jinsi Matara walikutana ana kwa ana na pasta Kanyari, kakake na marehemu Wahu;


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved