logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Prince Harry awasili nyumbani kwa Mfalme Charles London

Haimaanishi kuwa mkutano wa familia utaleta pamoja Prince Harry na Prince William.

image
na Davis Ojiambo

Habari07 February 2024 - 04:27

Muhtasari


  • • Magari ya SUV mawili yenye rangi nyeusi yalionekana yakiingia kwenye VIP Windsor Suite ya Uwanja wa Ndege wa Heathrow.

Mwanamfalme Harry amewasili Uingereza baada ya kusafiri kutoka Marekani kwenda kumuona Mfalme.

Anaonekana kuwa aliingia katika Clarence House, nyumba ya London ya Mfalme Charles na Malkia Camilla.

Magari ya SUV mawili yenye rangi nyeusi yalionekana yakiingia kwenye VIP Windsor Suite ya Uwanja wa Ndege wa Heathrow mapema mchana wa leo, yilipigwa picha yakiwasili kwenye makao ya kifalme, shirika la habari la PA linaripoti.

Vyombo vya habari vingine vinachapisha picha inayoonyesha Duke wa Sussex akiwasili katika moja ya magari.

Safari ya Prince Harry nchini Uingereza ni kuonana na babake baada ya kugunduliwa kuwa na saratani.

Lakini hiyo haimaanishi kuwa mkutano wa familia utaleta pamoja Prince Harry na Prince William.

Kulingana na vyanzo, kwa sasa hakuna mpango wa ndugu hao kukutana wakati Prince Harry yuko London.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved