logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Embu: Mwalimu ajiua na kuacha waraka kuzikwa siku ya Valentino, ex wake kusoma eulogy

Katika maelezo hayo, marehemu alieleza kwa nini aliamua kukatisha maisha yake.

image
na Davis Ojiambo

Habari08 February 2024 - 08:43

Muhtasari


  • • Barua ya kujitoa mhanga inayoaminika kuandikwa na Mwaniki ilipatikana ndani ya nyumba hiyo.
  • • Katika maelezo hayo, marehemu alieleza kwa nini aliamua kukatisha maisha yake.

Mwalimu mmoja wa kiume katika kaunti ya Embu amewashangaza wengi baada ya kujitoa uhai kisa kukataliwa na mpenzi wake wa zamani huku akiacha barua ya jinsi atakavyozikwa.

Kwa mujibu wa maelezo yake kwenye Facebook, Dennis Mwaniki maarufu kama Mkono, mwenye umri wa miaka 32 alianza kwa kuwaalika marafiki zake kwa shughuli yake kuu itakayofanyika siku ya wapendanao, Februari 14.

Bila kujua, kumbe alikuwa anatoa mwaliko kwa watu kuhudhuria mazishi yake kwani alikuwa tayari ameratibu kujitoa uhai kisa kukataliwa na aliyekuwa mpenzi wake.

"Wajumbe wa Jioni mkiwa na msongo wa mawazo mnahitaji tu rafiki mmoja wa kushiriki naye, wakati huo huo nawaalika kwenye shughuli yangu tarehe 14/2/2024 karibu wote."

Kamanda wa Polisi wa Kaunti ndogo ya Mbeere Kaskazini Eric Yego alisema MCA wa Nthawa Sammy Tito alitoa ripoti katika Kituo cha Polisi cha Siakago kwamba mwanamume mmoja hakuwa akipokea simu kutoka kwa marafiki na familia na alikuwa amejifungia ndani ya nyumba yake katika kijiji cha Nthangariri.

Yego alisema polisi walivunja mlango ili kuingia ndani ya nyumba hiyo na walimpata Mwaniki akiwa amekufa juu ya kitanda chake bila majeraha yoyote ya mwili isipokuwa damu na vitu vyeupe vinavyotoka puani.

Barua ya kujitoa mhanga inayoaminika kuandikwa na Mwaniki ilipatikana ndani ya nyumba hiyo. Katika maelezo hayo, marehemu alieleza kwa nini aliamua kukatisha maisha yake.

Aliagiza kwamba mazishi yake yafanyike Februari 14. Mwaniki alionyesha katika noti hiyo nambari ya simu ya mwanamke ambaye alimwagiza asome ujumbe wake.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved